JESHI la Polisi Tanzania limetangaza zawadi ya
Shilingi 150,000/= hadi 200,000/= kwa mtu au kikundi cha watu kitakacho toa
taarifa na kufanikisha kupatikana kwa watu wanochoma mabanda ya Nguruwe Mjini
Tunduru.
Zawadi hiyo imetangazwa na Kamanda wa polisi wa Mkoa wa
Ruvuma Bw. Deusdedit Nsemeki wakati akiongea katika kikao cha Viongozi wa
madhahebu ya Dini, Wazee maarufu kilichofanyika katika Ukumbi wa Klasta Mjini
hapa.
Akifafanua taarifa hiyo Kamanda Nsimeki alisema kuwa mtu au
kikundi kitakacho zawadiwa kitita hicho ni kile kitakacho toa taarifa zitakazo
fanikisha bila kuleta mashaka juu ya uhusika wa mlengwa katika matukio hayo ya
kuharibu mali
za wakristo yaliyojitokeza hivi karibuni Mjini humo.
Awali akiongea katika Mkutano huo kamishna kutoka Makao
Makuu ya jeshi la Polisi Tanzania ACP.Rashid Seyf alisema kuwa nia ya kamati
hiyo kuwaita makundi hayo ni kutafuta njia ya kuwapata wahalifu waliotekeleza
matukio hayo huku akiwaasa kutumia lugha ya kuneneza ili kuondoa makwazo kwa
kuwakumbusha machungu walioathiriwa na matukio hayo.
Akitoa tamko kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru kaimu
afisa Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Manfed Hyera alisema kuwa pamoja na kupiga
marufuku uuzaji na uoneshaji wa picha kutoka katika Cd,dvd ,hvc ,Flash na
Memori Card zote zinazo kashifu dini nyingine pia Kamati ya Ulinzi na Usalama
imeridhia kudhibitiwa muda wa ufungaji wa Vilabu vya pombe, waendesha Piki piki
na taxi kumaliza shughuli zao saa 5 kwa siku za kawaida na saa 6 siku za mwisho
wa wiki na sikukuu.
Alisema pamoja na maelekezo hayo pia uongozi wa wilaya hiyo umetoa
maelekezo yatayotakiwa kufuatwa na wahubiri wa mihadhara ya kidini pamoja na kuhakikisha kuwa kila muhubiri atafanya
mahubiri yake chini ya ulinzi wa Polisi na kwamba kutakuwa na timu itakayo
jihusisha na upigaji wa picha pamoja na kurekodi neno kwa neno kama ushahidi
endapo muhusika atakiuka maelekezo hayo.
Bw. Hyera aliendelea kueleza kuwa pia Wilaya hiyo imehimiza
kuanzisha ulinzi Shirikishi wa kutumia Sungungu huku wahudumu wa nyumba za
kulala wageni wakihimizwa kuandikisha kwa ufasaha majina na anuani za wageni
wote ikiwezekana wajiridhishe kwa kuomba na kusoma Vitambulisho vya wahusika zikiwa
ni juhudi za Serikali kudhibiti matukio ya aina hiyo.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho aliwataka
wananchi kujenga tabia za kutoa taarifa za matukio mabaya ili kuisaidia
serikali kuyadhibiti kabla hayajaleta madhala makubwa kwa jamii.
Wakichangia kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi walidai
kuwa hali hiyo imetokana na ulegevu wa serikali kwa kushindwa kusimamia
miongozo ya utengaji wa maeneo ya kuishi na kufugia hali ambayo ilitoa uhuru
kwa Wananchi kuweka Mifugo yao katikati Mji na makazi ya watu huku vitendo vya
uuzaji na uwekaji holela wa CD zinazo kashfu Dini nyingine kuwa ni miongoni mwa
vichochea vya matukio ya uchomaji wa Nguruwe, Mazizi, Nyumba, Magari pamoja na
uharibifu wa mali za watu.
.
Wakielezea masuala ya uendeshaji wa dini kwa
niaba ya waumini wa madhehebu ya kiislam Shehe Mkuu wa Wilaya hiyo Alhaji Waziri
Chilakwechi na Askofu Mkuu wa Jimbo la TUNDURU- MASASI pamoja na mambo mengine
waliunga mkono maamuzi ya kuzuiliwa kwa mikanda hiyo huku wakidai kuwa vitendo
hivyo vinavyofanywa na kikundi hicho kwa mwavuli wa dini mbali na kutia aibu jina
la Wilaya yao pia kinachafua haiba na uisilam na ukristo.
Bw. Rajab Rashid Mkwawa, Bw.
Rashid Mkanyasine, Bi. Janneth Amani wakamweleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa
kitendo cha Serikali kushindwa kuwakamata wahalifu hao kunatokana na suala hilo kuhusishwa na UDINI
hali ambayo kila mtu anaogopa kulisemea.
Bw. Abdalah Kawanga, Ado
Makanya pamoja na kuunyooshea vidole udhaifu wa vyombo vya Usalama hususani
jeshi la Polisi ambalo hivi sasa limepoteza maadili kutokana na watendaji wake
kuanza kutoa siri na kuwataja kwa wahalifu wanaotoa taarifa hizo za siri pia
waliwatuhumu wazazi kwa kufumbia macho Lugha ambazo zimekuwa zikitumika na
vijana wao kuwa endapo zitadhibitiwa ni rahisi kuwatambua wahusika.
Kufuatia hali hiyo wananchi hao
wakaitaka Serikali kupitia Mkuu huyo wa Wilaya hiyo kutumia mamlaka waliyopewa
kwa kuanza kuwachukulia hatua watendaji wote wanaoshimdwa kuwajibika ili
kujenga nidhamu ya utendaji kazi na kurejesha imani ya upatikanaji wa huduma
bora kwa jamii.
No comments:
Post a Comment