Mmoja kati ya wafugaji wang'ombe jamii ya kimang'ati
Serikali Mkoani Ruvuma imetoa mwenzi mmoja kwa Wafugaji wa jamii za
Kisukuma na Wamang‘ati walioingiza Ng’ombe wao kiholela bila kufuata utaratibu
kuondoka Mkoani humo vinginevyo Sheria itafuata mkondo wake ikiwa ni pamoja na
kufanyika kwa Oparesheni ya kuwafukuza.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said thabity Mwambungu,
wakati akiongea na Viongozi wa Serikali Wilayani Tunduru kutokana ukiukwaji wa
taratibu za kuingiza wanyama hao bila kufuata taratibu hali ambayo inaweza
kuleta madhala na kuzuka kwa mapigano makubwa baina ya wakulima na wafugaji.
Bw. Mwambungu akatumia nafasi hiyo kumtaka Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Chander
Nalicho na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw.Albert Nehata kusimamia
zoezi hilo na kuhakikisha kuwa Watendaji wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji,
Maafisa tarafa kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa nguvu zao zote utekelezaji wa
tukio hilo na kwa kiongozi anaye jiona kuwa hata mudu basi aachie dhamana hiyo
aliyopewa na Serikali.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya
Tunduru ililidhia kupokea Ng’ombe elfu kumi tu (10,000) na wafuagaji hao kutengewa
maeneo katika kata za Mhuwesi, Masonya na Ngapa lakini cha kushangaza wafugaji
hao wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku na kuenea katika maeneo yote ya Wilaya
hiyo.
Wanachi wa wilaya ya Tunduru wamelalamika kuona wafugaji hao kuendelea
kuvamia hadi katika hifadhi ya Taifa ya Selous, na hifadhi zamapori tengefu amabazo
hutumika katika bishara ya uwindishaji wa Kitaali zilizopo katika maeneo mbali
mbali ya vijiji vilivyo Wilayani humo huku kukiwa na makatazo ya kuwazuwia
wanachi kuingia na hata kulima.
kundi kubwa la ng'ombe katika poli la hifadhi ya selous
No comments:
Post a Comment