Shekh mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania Wilayani Tunduru Alhaji waziri
Chilakweche
Na,Steven
Augustino,Tunduru
Watu
wanaodhaniwa kuwa ni Waislamu wenye msimamo Mkali wa Dini wamemvamia na kumpiga
Shekh Mkuu wa Baraza la Waislamau Tanzania Wilayani Tunduru Alhaji waziri
Chilakweche na kumsababishia maumivu makali.
Kabla ya
tukio Shekh huyo alifatwa nyumbani kwake
na vijana na kumuomba watoke nae nje ya eneo la
nyumba yake wakidai kuwa wanaomba awasaidie kusuhisha Mgogoro uliokuwa umezuka
katika msikiti wa Kitumbini katika Mtaa huo.
Sambamba na
tukio hilo pia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajab Abdalah (17)
Amelazwa katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru akiwa hajitambui
baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu ambao walidaiwa kukimbilia
katika tukio la shambulizi la Shekh Chilakwechi.
Mashuhuda
wa tukio hilo walidai kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa manane ambapo
katika madai yao vijana hao walimtuhumu Alhaji Chilakwechi kuwa amekuwa
akishiriki na kula vyakula vya wakirsto.
Akiongea kwa
taabu alihaji chilakwechi alidai hakuwa
na ubaya nao na wala hajwahi kugombana na mtu hali ambayo inamshangaza na anaiomba
Serikali ifuate mkondo wake kwa wahusika.
kuhusu
tuhuma za yeye kushiriki katika shughuli za dini katika madhehebu ya wakristo
alidai kuwa hicho siyo kitu cha ajabu kwa viongozi wa dini na kuongeza
kuwa wao kama viongozi wa dini huwa na ushirikiano na huitana na
kutembeleana kwa vile dini hailuhusu uhasama miongoni mwao.
Kamanda
wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedth Nsimekli amedhibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kueleza kuwa jeshji la polisi linaendelea na uchunguzi ili kujua
kiini cha tukio hilo.
Aidha
kamanda Nsimeki alikiri pia kufahamu matukio ya udini yanayo endelea Wilayani
Tunduru nakuongeza kuwa jeshi limejipanga kuhakikisha kuwa wanadhibiti vitendo
hivyo.
No comments:
Post a Comment