Na Steven
Augustino,Tunduru
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema Serikali itahakikisha
wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuanzia sasa wanarejea na kuanza kuishi maisha ya
amani na utulivu kutokana na hatua kali zitakazo chukuliwa kwa watu ambao
wamekuwa wakichochea vurugu,
Akizungumza katika mikutano tofauti mjini Tunduru alipokutana viongozi wa
dini, watumishi wa halmashauri na baadaye katika Mkutano wa hadhara
uliofanyika katika viwanja vya Baraza la Idd mjini Tunduru.
Akifafanua taarifa hiyo Bw. Mwambungu alisema kuwa vitendo vya Kumpiga
Shekh Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Alhaji Waziri Chilakwechi (75), Uchomaji wa
Nguruwe, Magali na uhalibifu wa mali za wananchi wa Wilayani humo,
Ni uhalifu unaofanywa na wahuni ambao wanatumia mwamvuli wa Dini na kwa kujiita waislamu wenye msimamo
mkali, hivyo kuanzi sasa watasakwa na kupelekwa katika mikono ya sheria.
Aidha Bw. Mwambungu akatumia nafasi hiyo kwa viongozi wa Serikari Mkoani
Ruvuma kuwataka wachukue hatua za kisheria kwa wanaohatalisha amani na kuweka
mikakati ya kuzuwia matukio yanayojitokeza katika maeneo yao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw Chande Nalicho akitoa taarifa za vitendo
vya matukio yaliyosababisha tahaluki miongoni mwa jamii Wilayani Tunduru, Amesema
kuwa Wilaya yake imejipanga kuhakikisha kuwa wahalifu hao wanachukuliwa hatua
kulingana na makosa yao.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedit
Nsimeki alisema kuwa tayali Jeshi hilo linawashikilia watu 6 ambao alidai kuwa
taratibu za kuwapeleka mahakamani zinaendelea.
Katika taarifa hiyo Kamanda Nsimeki aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
Shaibu Said(22), Rajab Abdalah (17),Bakali maloya (22) Rajab hasan (22),Ally
Kapopo (27) na Seleman Likoloma(20)ambao kwa pamoja walidaiwa
kumshambulia Shekh Mkuu wa Wilaya hiyo.
Kufuatia hali hiyo kamanda Nsimeki pia akatumia nafasi hiyo kuwaomba
wananchi kulisaidia jeshi hilo kutoa taarifa za wahalifu waliotekeleza matukio
hayo na kusababisha tahaluki kwa jamii.
No comments:
Post a Comment