JUMLA
ya Magunia 224 ya mahindi, Mpunga na Maharage mali ya wakulima 10 wa
Kijiji cha Mbati mashambani yameteketea kutokana na kuchomwa kwa moto
uliozuka katika eneo hilo na kuwasababishia hasara ya kukosa chakula na
efdha ya kujikimu.
Sambamba
na tukio hilo pia moto huo umeteketeza Nyumba Nane pamoja na mali
zlizokuwemo ndani zikiwemo Nyumba tano za famila moja pamoja na majirani
waliokuwa wakilima wa kijiji hicho.
Taarifa
za tukio hilo zinaeleza kuwa moto huo ulizuka majira ya saa nane mchana
ambapo katika tukio hilo wakulima hao walikuwa wameenda kufuata
mahitaji Kijijini Mbati na kuacha mali hizo zikiwa na msimamizi mmoja tu aliyefahamika kwa jina la Bw. Said Nyenje hali ambayo ilimuwia vigumu kuziokoa.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo wakulima walioathiriwa na tukio hilo ni
Bw.Rashid Ramadhani aliyeunguliwa na maghala mawili alimo kuwa ametunza
magunia 52 ya mahindi ya Chakula na Biashara.
Wengine
walio athiriwa na mkasa huo ni Bw.Said Nyenje aliye unguliwa Gunia 32
za Mahindi,Bi. Mwanabibi Hashimu gunia 18, Bw. Amanzi Ngaunje magunia 30
na Bw. said Abdalah gunia 19.
Taarifa
hiyo pia imewataja Bw. Bakari Chiganisya magunia 5, Bi. Mwanabibi
Chalamanda magunia 8 na Bi. Fatuma Musa aliyeunguliwa na debe 37 za
mahindi.
Aidha moto huo pia uliteketeza Debe 70 za Mpunga na maharage zikiwemo Debe 56 za mpunga na Maharage debe 14 mali ya wakulima hao
Miongoni
mwa mashuhuda wa tukio hilo Bw. Mohamed Magawa alisema kuwa kutokana na
Moto huo kuwa mkubwa na kasi walishindwa kuuthibiti na kuendelea
kushuhudia wakati mali zao zikiteketea.
Taarifa
iliyotolewa na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho
Bw.Athuman Ntila mbali na kukiri kuwepo kwake walisema kuwa tukio hilo
limewaathiri kwa kiasi kikubwa wakulima hao pamoja na mfanya biashara
aliyekuwa amefanya nao mkataba wa kuyanunua mahindi hayo baada ya
kuyakusanya.
Akiongea
kwa uchungu kwa niaba ya wahanga hao Bw.Rashid Ramadhani alieleza kuwa
hadi sasa hakuna mtu wanaye muhisi na wala hawatarajii kupeleka kesi
hiyo Polisi kwa madai kuwa watachunguza wenyewe na kuchukua hatua hata
kwa njia za giza akiashiria kuwa wanampango wa kwenda kuloga kwa
wataalamu waliopo Nchi jirani ya msumbiji.
Juhudi
za kuwatafuta Mtendaji wa Kijiji hicho Bw. Alli Chandu na Diwani wa
kata hiyo Bw. Burhan nakaanje ili kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa
matunda kutokana na Viongozi hao kudaiwa kuwa wapo katika safari za
kikazi.
No comments:
Post a Comment