Na Steven Augustino, Tunduru
SERIKALI Wilayani Tunduru
Mkoani Ruvuma Imeahidi kuunda Tume itakayo saidia kufuatilia na kudhibiti Bei
ya Bidhaa zikiwa ni juhudi za Serikali kuwapunguzia mzigo walaji.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa
Wilaya hiyo Bw. Chande Nalicho wakati akiongea na Wadau wa Maendeleo katika
kikao kilichofanyika katika Viwanja vya Ikulu Ndogo mjini hapa.
Akifafanua taarifa hiyo Bw. Nalicho
alisema kuwa maamuzi hayo yamefuatia kuwepo kwa mlipuko mkubwa wa Bei za Bidhaa
hali ambayo imekuwa ikiwawia vigumu wananchi kumudu kupata mahitaji yao.
Alisema katika tume hiyo
ambayo itawashirikisha Afisa Biashara na Mchumi wa halmashauri hiyo pamoja na mambo mengine viongozi hao
watatakiwa kufanya kazi ngumu ya kuzungumza na Wafanyabiashara wote zikiwa ni juhudi
za kumsaidia mlaji na kumwezesha kupata bidhaa hizo kwa bei inayo endana na
ubora wa bidhaa husika.
Bw. Nalicho aliendelea
kufafanua kuwa endapo hali hiyo haitadhibitiwa ipo hatari ya Wafanyabiashara
hao kuendelea kujinufausha kwa kupata faida kubwa huku mlaji akipata bidhaa
hiyo kwa bei aghali na kumfanya ashindwe kumudu kufanya shughuli nyingine za
maendeleo.
“ hali hii inabidi idhibitiwe
kwa taarifa zilizopo zinzonesha kuwa Bidhaa zote zilipanda miaka ya 1994/1995
wakati Wilaya hiyo ilipo kuwa na mlipuko wa upatikanaji wa madini ya Vito”
alisema Dc, Nalicho .
Sababu nyingine zilizotajwa
kuwa zilikuwa ni kikwazo cha upandaji wa bei za bidhaa hizo katika kipindi
hicho kuwa ni ubovu wa barabara kutoka Dar- Es Salaam kupitia Kibiti Lindi hali
amabyo ilikuwa ikwafanya kufuata Bidhaa zao kupitia njia ya Songea – Dar Es
Salaamu na baadae Songea – Tunduru lakini hivi sasa Bidhaa zao hufika kwa
urahisi baada ya barabara ya Kibiti Lindi kufunguka.
Alisema baada ya kufunguka
kwa barabara hiyo yenye umbali wa
kilometa 800 kutoka Jijini Dar es salaam kupitia Kibiti Lindi wafanyabiashara
wote wamekuwa wakipitisha bidhaa zao huko tofauti na zamani ambapo walikuwa
wakipitia Songea ambako kulikuwa na umbali za zaidi ya kilometa 1264 na kwamba
hivi sasa wafanyabishara hao wanatakiwa kuwa na roho za kibinadamu na kuondoa
kisingizio cha ukubwa wa Ghalama za usafiri kwa lengo la kutaka kujilimbikizia
faida.
Alisema kutokana na hali hiyo
wananchi hawakuwa na mahali pa kukwepea lakini hivi sasa madini hayo yamekwisha
hivyo wafanyabiashara pia wanatakiwa kutambua hali hiyo na kuanza kuuza bidhaa
zao kwa bei za kawaida na siyo kujilimbikizia faida maradufu kama
wanavyo fanya sasa.
Awali akiwasilisha taarifa ya
malalamiko hayo katibu wa Umoja wa makanisa Wilayani Tunduru Padre Dominick
Mkapa alitolea mfano Bidhaa za Viwandani yakiwemo mabati, saluji na hata vinywaji
ambavyo bei zake zipo juu hali ambayo imekuwa ikwawia vigumu wananchi hata
kuanzisha shughuli za ujenzi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Mfuko wa saluji
umeuzwa kwa Bei ya kati ya Tsh. 24,000 na Tsh. 26,000 , Bati Tshi 22,000 hadi
Tsh. 28,000 huku bei ya Soda pia ikiwa ni Tsh. 1,000/= na kilo moja ya Sukali
ikiuzwa kwa yati ya Tsh. 2200 na 2400.
Akizungumzia hali hiyo kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya hiyo Bw. Rashidi Mandoa mbali na
kukiri kuwepo kwa hali hiyo alisema kuwa halmashauri yake ipo tayari kuwatoa
wataalamu hao.
Alisema wakati wa utekelezaji
wa zoezi hilo watasaidia kufanya utafiti bei kwa kufanya malinganisho ya Bei za
Bidhaa hizo katika Wilaya na miji jirani na baadae kutoa ushauri kwa
wafanyaabishara wa Wilaya hiyo
No comments:
Post a Comment