Na Steven Augustino, Tunduru
VIONGOZI
wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) katika Kata ya Ligunga
Wilayani Tundudru Mkoanai Ruvuma umejiengua katika chama hichona
kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM.
Pamoja
na kukihama chama hicho na kukabidhiwa kadi mpya za chama cha
Mapinduzi,Viongozi hao wametamba kukisambaratisha kabisa chama hicho na
kuhakikisha kuwa kata hiyo ambayo inaongozwa na Diwani wa Chadema kwa
miaka 7 sasa inarejea mikononi mwa chama tawala katika uchaguzi mkuu
ujao.
Tukio lilijitokeza Katika Hafla ya kumakaribisha na kumpongeza Bw. Ajili kalolo kwa
kuwa mshindi wa nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) taifa (NACK) iliyofanyika katika Kijiji cha Jakika
Wilayani humo.
Wakitangaza
uamzi huo aliyekuwa Mwenyekiti Chadema Kata ya Ligunga Mwenye Akwitanda
(Bw.Mohamed Msusa )alisema kuwa yeye pamoja na viongozi wenzake amabo
walikihama chama cha Mapinduzi mwaka 2000 kutokana na kero za ubabe na
sera kandamizi za viongozi walio ondolewa ndani chama hicho katika
uchaguzi uliopita na kwamba kurudi kwao kumetokana na kuamini kuwa hivi
sasa chama hicho kupitia mjumbe huyo kitaendesha bila ubaguzi.
Upande
wa Bw.Dinani Nambala aliyekuwa na nyadhifa za Mwenyekiti wa Vijana wa
Chadema katika kata hiyo na Mjumbe wa mkutano Mkuu Chadema Taifa alisema
kuwa kero kubwa ya wanachama hao kuihama CCM mwaka 2000 ilitokana na
Uongozi wa Wilaya hiyo kukata Jina la Mgombea ambaye alikuwa ameshinda
katika kura za maoni na kuwachaguliz mgombea.
Akifafanua
taarifa hiyo Bw. namala alisema kuwa katika uchaguzi huo Bw. Kazembe
Said alishinda kwa kupata kura 80 lakini kutokana na ubabe wa uongozi wa
CCM wilaya walipandikiza jila la Bw. Omar Kiinge ambaye katika mkutano
huo wa uteuzi alipata kura 12 hali ambayo iliwasukuma kuingia msituni na
kumsaidia Bw Kazembe ambaye walimshauri ajiunge na Chadema na kuibuka
mshindi katika chaguzi za mwaka 2000 na 2010.
Wengine
waliojiengua kutoka chadema ni mjumbe wa baraza la wazizi Wilaya Mwenye
Akumgambo, pamoja na waliokuwa wapiganaji na wafadhili wakuu wa Chadema
Bw. Hasan Ndalanga, Bi. Mwanahawa Msham.
Akiongea katika hafla hiyo pamoja na kuwapongeza viongozi hao kwa kujenga imani
na kurejea katika chama chao mjumbe huyo ambaye pia ni Sultan wa kanda
ya Kusini Bw. Ajili Kalolo pamoja na mambo mengine aliomba ushirikiano
kwa wanachama na wakereketwa wa chama cha mapinduzi kukisaidia chama
hicho ili kuludisha imani kwa wananchi na kukihakikishia ushindi katika
chaguzi zijazo.
Aidha
Bw. kalolo aliwapongeza wajumbne wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya kwa
kumchagua kuwa mjumbe wa Neck Taifa na kuahidi kuwa yupo tayali kupoteza
maisha katika kutetea maslahi ya chama hicho na akatumia nafasio hiyo
kuomba ushirikiano kwa viongozi wote pindi akatapo tembea na kuhamasisha
chama katika matawi, mashina,Vijiji,kata na Wilaya zikiwa ni juhudi za kukijenga upya chama hicho.
Awali akitoa taarifa za Ushindi huo mshauri mkuu wa Mneck huyo aliyechaguliwa kwa kupata kura 889,
Bw. Sekula Matumla alidai kuwa katika kipindi chote cha uongozi wake
atamshari kuondoa makundi ndani ya Chama hicho ili kurejesha imani kwa
wananchi na kuwafanya kujiunga na CCM na ikiwezekana doa la upinzani
katika Wilaya hiyo liondoke kabisa.
Naye Katibu
wa CCM Wilaya ya Tunduru Bw. ramadhan Amer katika hotuba yake
alimweleza Bw. Kalolo kuwa nafasi hiyo ameipata kutokana na kujitoa
kwake ndani ya chama na kuongeza kwa kuwahimiza viongozi wote kuwajibika
katika nafasi zao ili kujenga chama imara kitakacho pata ushindi katika
chaguzi za mwaka 2014 na uc haguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment