Na shekhan mzaina
Katibu wa UWT Taifa MB.AMINA NASSORO MAKILAGI akiotekasalimiana na wananchi wa kjiji cha mchoteka kata ya mchoteka.
Katibu wa
jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi CCM na mmbunge wa viti maalum AMINA NASSORO MAKILAGI amemaliza ziara iliyodumu
kwa siku tatu katika wilaya ya Tunduru iliyoanza tarehe 1.10.2013 hadi tarehe
3.10.2013.
Katibu wa UWT Taifa MB.AMINA NASSORO MAKILAGI akihutubia wananchi wa kata ya namihungo wilayani Runduru mkoani Ruvuma.
Pichani wanakijiji cha nakapanya wakisikiliza hotuba ya Katibu wa UWT Taifa na MB. viti maalum AMINA NASSORO MAKILAGI
Wakati wa
ziara yake wilayani humo yenye malengo mbalimbali ya chama na serikali amewataka wananchi hususani akinamama
kuwapuuza baadhi ya wanasiasa wanaochochea vurugu katika nchi yetu ya Tanzania
kwani amani iliyopo hapa nchini haikupatikana hivihivi bali lipatikana kwa
jasho na wananchi hawanabudi kuilinda amani hiyo,hata hivyo AMINA MAKILAGI amewasihi
wanawake wa wilayahiyo kuwa mstari wa mbele kulinda amani nchini kwani wakati
wa vurugu akinamama na watoto ndio waathirika wakubwa
.
Akizungumzia
tatizo la maji ambalo ni tatizo sugu kwamaeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo wilaya ya Tunduru amesema serikali inamikakati kabambe ya
kutatua tatizo hilo wilayani humo kwani katika bajeti ya mwaka 2013/2014
serikali imezamilia kupeleka huduma ya maji vijijini kwa kuongeza bajet ya
wizara ya maji ili kujiondoa na utegemezi wa wahisani kwa kiasi kikubwa katika
utekelezaji wa miradi ya maji na kata za
Nakapanya na Namihungo wilayani tunduru zitanufaika na mpango huo.
Kwa kutambua
changamoto zilizopo katika sekta ya afya katibu huyo wa UWT taifa ameahidi
kutoa msaada wa vitanda vine vya kujifungulia akinamama vyenye thamani ya shilingi
milioni mbili na lakinane kwa vituo vya
afya vya Nakapanya na Mchoteka kwa mgawanyo sawa wa vitanda viwili kwa kila
zaanati hizo.
wanachama wapya wa chama cha mapinduzi CCM wakiapishwa wakati wa mkutano wa Katibu wa UWT Taifa MB.AMINA NASSORO MAKILAGI
Katika ziara
yake hiyo wilaya humo UWT imeongeza wanachama wapya 127 katika kata tano za wilaya ya Tunduru huku wanachama sita
kutoka chama cha wananchi CUF wamerudisha kadi na kujiunga na chama cha
mapinduzi CCM.
No comments:
Post a Comment