Mwenyekiti wa umoja wa vijana
chama cha mapinduzi CCM Khalfan Kigwenembe ametoa ahadi hiyo ya kuchangia
madawati baada ya risala ilyosomwa shuleni hapo na Mwalimu mkuu wa shule Bi
Otilia Mbano kuonesha shule inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa madawati na
kusababisha wanafunzi hao kukaa chini wakati wa masomo
Akipokea risala kutoka kwa mwl/mkuu
Aidha aliwataka wazazi wa
watoto hao kuhakikisha watoto wao wanajiunga na Darasa la kwanza mapema
ifikapo mwaka 2013 ilikuendeleza masomo
yao nakufika mbali kielimu huku akitoa mchango wa madaftari kwa wahitimu wote
ili kuwapunguzia wazazi mzigo wa kununua vifaa vya kujifunzia pindi watakapo
jiunga na darasa la kwanza,hata hivyo bwn:Kigwenembe amehaidi kuwa tafutia eneo
la ujenzi wa shule hiyo kwani kwasasa shule hiyo inatumia majengo ya kupanga.
Akikabidhi vyeti kwa wahitimu
katika mahafari ya tisa ya
shule ya mtakatifu teresia iliyopo bombambili mjini Songea wanafunzi 48
wamehitimu elimu ya awali na kutunukiwa vyeti.
Nibaadhi ya wazazi wakiangalia kwaya kutoka kwa wahitimu ambao ni watoto wao.
No comments:
Post a Comment