Sunday, October 28, 2012

Serikali Mkoani Ruvuma imetoa mwenzi mmoja kwa Wafugaji wa ng'ombe kuhama mkoani Ruvuma


Mmoja kati ya wafugaji wang'ombe jamii ya kimang'ati

Serikali Mkoani Ruvuma imetoa mwenzi mmoja kwa Wafugaji wa jamii za Kisukuma na Wamang‘ati walioingiza Ng’ombe wao kiholela bila kufuata utaratibu kuondoka Mkoani humo vinginevyo Sheria itafuata mkondo wake ikiwa ni pamoja na kufanyika kwa Oparesheni ya kuwafukuza.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said thabity Mwambungu, wakati akiongea na Viongozi wa Serikali Wilayani Tunduru kutokana ukiukwaji wa taratibu za kuingiza wanyama hao bila kufuata taratibu hali ambayo inaweza kuleta madhala na kuzuka kwa mapigano makubwa baina ya wakulima na wafugaji.
Bw. Mwambungu akatumia nafasi hiyo kumtaka Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Chander Nalicho na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw.Albert Nehata kusimamia zoezi hilo na kuhakikisha kuwa Watendaji wa Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji, Maafisa tarafa kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa nguvu zao zote utekelezaji wa tukio hilo na kwa kiongozi anaye jiona kuwa hata mudu basi aachie dhamana hiyo aliyopewa na Serikali.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ililidhia kupokea Ng’ombe elfu kumi tu (10,000) na wafuagaji hao kutengewa maeneo katika kata za Mhuwesi, Masonya na Ngapa lakini cha kushangaza wafugaji hao wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku na kuenea katika maeneo yote ya Wilaya hiyo.
Wanachi wa wilaya ya Tunduru wamelalamika kuona wafugaji hao kuendelea kuvamia hadi katika hifadhi ya Taifa ya Selous, na hifadhi zamapori tengefu amabazo hutumika katika bishara ya uwindishaji wa Kitaali zilizopo katika maeneo mbali mbali ya vijiji vilivyo Wilayani humo huku kukiwa na makatazo ya kuwazuwia wanachi kuingia na hata kulima.
Afisa Kilimo na Migfugo wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chiza Malando mbali na kukiri  kwa uingizaji holela wa mofugo hiyo alisema kuwa hivi sasa Wilaya ya Tunduru imeonekana kuelemewa na wingi wa mifugo hiyo,kwani hadi sasa Wilaya hiyo inakadiliwa kuwa na zaidi ya Ng’ombe 40,000 kutoka kwa wafugaji hao tofauti na malengo ya kuwa na Ng,ombe 10,000 
 kundi kubwa la ng'ombe katika poli la hifadhi ya selous

Thursday, October 25, 2012

AJALI IMETOKEA MAENEO YA BOMBAMBILI NA KUSABABISHA KUPASUKA USONI KWA DEREVA PIKIPIKI

Gari lililogongwa
Ajali hii imetokea maaneo ya white house jirani na ofisi za Tbc songea majira ya saa 5:20 jioni ,
Ajal hii imehusisha dereva pikipiki (yeboyebo) na gari aina ya Vitara iliyokuwa ikitokea msamala ikielekea mjini.
Chanza cha hajali hiyo kwa mashuhuda walioiona wamedai dereva wa gari aina ya vitara alisimama gafla kwenye matuta badala ya kupunguza mwendo.
Ndipo kijana huyo ambaye ni dereva pikipiki(yeboyebo) alipomva na kumgonga kwa nyuma na kuchanika usoni, Kijana huyo amepelekwa hospital ya mkoa wa Ruvuma kupata matibabau.
Pia wamesema dereva wa Gali hilo ambaye akufahamika jina kwa haraka alikuwa akiendesha gari huku amelewa ,
Aidha wamelaana juu ya hawa madereva wanaoendesha magari wakiwa wamelewa kwani wanasababisha ajari nyingi barabarani pia wanaiomba serikali kuchukua mkondo wake kwa hawa madereva wanaoendesha huku wamelewa.
Ilikupunguza ajali nyingi barabarani pia nakuwataka hawa madereva wa pikipiki(Yeboyebo) kuendesha kwa umakini wawapo barabarani kwani wamekuwa wakiendesha kwa kutofata sheria za barabarani.
Huyu mzee alievaa shati la mistari ndie mwenye gari
  Askari wa Barabarani wakiwa eneo la tukio
Moja ya mashuhuda wakiangalia ajari

Moja ya madereva pikipiki(yeboyebo) wakitoa ushirikiano kwa Askari wa barabarani

Serikali Mkoani Ruvuma imeapa kuwasaka kwaudi na uvumba wote wanaotaka kuvunja Amani


Na Steven Augustino,Tunduru                                                             
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema Serikali itahakikisha wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuanzia sasa wanarejea na kuanza kuishi maisha ya amani na utulivu kutokana na hatua kali zitakazo chukuliwa kwa watu ambao wamekuwa wakichochea vurugu,

Akizungumza katika mikutano tofauti mjini Tunduru alipokutana viongozi wa dini, watumishi wa halmashauri na baadaye katika  Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Baraza la Idd mjini Tunduru.
Akifafanua taarifa hiyo Bw. Mwambungu alisema kuwa vitendo vya Kumpiga Shekh Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Alhaji Waziri Chilakwechi (75), Uchomaji wa Nguruwe, Magali na uhalibifu wa mali za wananchi wa Wilayani humo,

Ni uhalifu unaofanywa na wahuni ambao wanatumia mwamvuli wa Dini na kwa kujiita waislamu wenye msimamo mkali, hivyo kuanzi sasa watasakwa na kupelekwa katika mikono ya sheria.
Aidha Bw. Mwambungu akatumia nafasi hiyo kwa viongozi wa Serikari Mkoani Ruvuma kuwataka wachukue hatua za kisheria kwa wanaohatalisha amani na kuweka mikakati ya kuzuwia matukio yanayojitokeza katika maeneo yao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw Chande Nalicho akitoa taarifa za vitendo vya matukio yaliyosababisha tahaluki miongoni mwa jamii Wilayani Tunduru, Amesema kuwa Wilaya yake imejipanga kuhakikisha kuwa wahalifu hao wanachukuliwa hatua kulingana na makosa yao.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedit Nsimeki alisema kuwa tayali Jeshi hilo linawashikilia watu 6 ambao alidai kuwa taratibu za kuwapeleka mahakamani zinaendelea.
 Katika taarifa hiyo Kamanda Nsimeki aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shaibu Said(22), Rajab Abdalah (17),Bakali maloya (22) Rajab hasan (22),Ally  Kapopo (27) na Seleman Likoloma(20)ambao kwa pamoja walidaiwa kumshambulia Shekh Mkuu wa Wilaya hiyo.

Kufuatia hali hiyo kamanda Nsimeki pia akatumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kulisaidia jeshi hilo kutoa taarifa za wahalifu waliotekeleza matukio hayo na kusababisha tahaluki kwa jamii.

Wednesday, October 24, 2012

Dkt.Bilal Afungua Mkutano Mkuu Wa Vyuo Vikuu Afrika Mashariki

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustine, Dkt. Charles Kitima, wakati alipokuwa akitembelea kukagua mabanda ya maonyesho baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki.
-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Umoja wa Mawaziri wa Afrika Mashariki, Musa Sirima, wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Vyuo Vikuu  unaoshirikisha pia Kamisheni ya Biashara ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu jijini Arusha na unajumuisha wakuu na wawakilishi wa vyuo mbalimbali vya elimu ya juu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Picha na OMR

Chanzo  Mjengwa blog

Shekh Mkuu Wa Wilaya ya Tunduru achezea kichapo

 
Shekh mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania Wilayani Tunduru Alhaji waziri Chilakweche
Na,Steven Augustino,Tunduru
Watu wanaodhaniwa kuwa ni Waislamu wenye msimamo Mkali wa Dini wamemvamia na kumpiga Shekh Mkuu wa Baraza la Waislamau Tanzania Wilayani Tunduru Alhaji waziri Chilakweche na kumsababishia maumivu makali.
Kabla ya tukio Shekh huyo alifatwa  nyumbani kwake na vijana na kumuomba watoke nae nje ya eneo la nyumba yake wakidai kuwa wanaomba awasaidie kusuhisha Mgogoro uliokuwa umezuka katika msikiti wa Kitumbini katika Mtaa huo.
Sambamba na tukio hilo pia kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Rajab Abdalah (17)  Amelazwa katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Tunduru akiwa hajitambui baada ya kushambuliwa  kwa mapanga na watu ambao walidaiwa kukimbilia katika tukio la shambulizi la Shekh Chilakwechi.
  Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa manane ambapo katika madai yao vijana hao walimtuhumu Alhaji Chilakwechi kuwa amekuwa akishiriki na kula vyakula vya wakirsto. 
Akiongea kwa taabu alihaji chilakwechi alidai  hakuwa na ubaya nao na wala hajwahi kugombana na mtu hali ambayo inamshangaza na anaiomba Serikali ifuate mkondo wake kwa wahusika.
 kuhusu tuhuma za yeye kushiriki katika shughuli za dini katika madhehebu ya wakristo alidai kuwa hicho siyo kitu cha ajabu kwa viongozi wa dini na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa dini huwa na ushirikiano na huitana na kutembeleana kwa vile dini hailuhusu uhasama miongoni mwao.
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedth Nsimekli amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshji la polisi linaendelea na uchunguzi ili kujua kiini cha tukio hilo.
Aidha kamanda Nsimeki alikiri pia kufahamu matukio ya udini yanayo endelea Wilayani Tunduru nakuongeza kuwa jeshi limejipanga kuhakikisha kuwa wanadhibiti vitendo hivyo.
  Rajab Abdalah (17)

Friday, October 19, 2012

Wakazi Wa Iringa, Waendelea Kutoa Maoni Kuhusu Katiba Mpya

Heny Mkenja, akijaza fomu maalumu ya maoni ya katiba mpya 
Baadhi ya wakazi wa Iringa ,kata ya Mivinjeni wakifatilia maoni ya wenzao kwa makini
Christina Mgongolwa, mkazi wa kata ya mivinjeni amependekeza kwamba katika katiba mpya ijayo,somo la maarifa ya nyumbani lipewe mhimu wake

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki akabidhi tuzo kwa Asasi zinazotoa msaada wa kisheria nchini

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki akizindua awamu ya pili ya kuzisaidia kifedha Asasi zinazotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini katika hafla iliyofanyika jana, jijini Dar Es Salaam.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. angellah Kairuki akikabidhi tuzo ya fedha kwa moja ya Asasi zilizopata tuzo hizo jana jijini Dar Es Salaam. Katikati anayeshuhudia ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Othman Makungu.

Magari Ya Serikali Yanayotumia Namba Binafsi Kusakwa

 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (waliokaa mbele wapili kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kusisitiza  utaratibu wa usajili wa magari
 ya Umma unafuatwa na kutafanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote.Serikali imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba  za kiraia, yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma .  Baada ya hapo Operesheni hiyo iitakamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma,Vilevle kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT,JW, DFP, CW, SM na ,SU.Hadi sasa serikali imesajili vyombo vya moto,123,431 yakiwemo magari,,pikipiki,bajaj na mitambo ya umma (pichani anaefuatia mwenye sare za polisi) ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani katika jeshi la Polisi  nchini Kamanda James Mpinga). (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).



 
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiteta jambo na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani James Mpinga ili magari ya umma yaliyo na namba za kiraia yarejeshwe kwenye namba  stahiki za magari ya Umma kabla ya oparesheni ya kamatakamata kuanza.  (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO)

Rais Amteua Mwenyekiti Wa Bodi Ya Wakurugenzi TBC

 Na . Veronica Kazimoto – MAELEZO 

 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete amemteua Prof. Mwajabu Possi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 8 Octoba, 2012. Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amewateua wajumbe mbalimbali wa bodi hiyo ambao ni Dkt Mariam Nchimbi, Gideoni Mbalase, Prof.

 Elizabeth Kiondo na Balozi Kassim Mwawando. Wajumbe wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Assah Mwambene, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu, Mkurugenzi wa Idara ya Habari -MAELEZO Zanzibar Omary Chunda pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Clement Mshana. 

Wakati huo huo Waziri Mkangara amemteua Christopher Gachuma kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya. Aidha amewateua Pendo Malebeja, William Erio, Richard Ndassa, Lina Kessi, Leornard Thadeo na Allen Alex kuwa wajumbe wa bodi hiyo.

Thursday, October 18, 2012

PICHA ZA HARUSI YA MTANGAZAJI WA RADIO JOGOO NA WAPAMBE WAO WATANGAZAJI WA TBC ILIYO FANYIKA KATIKA UKUMBI WA FAMILIA TAKATIFU BOMBAMBILI

Bw.Harusi Francis Sengo wa upande wa kulia akiwa na mpambe wake Gerson Msigwa

                                                 Bw.Harusi akimlisha keki Bi.Harusi

                             Bw.harusi Francis Sengo na Bi.harusi Jacline Mkomange wakiwa katika pozi
Bi.harusi akikabidhi keki upande wa kiumeni
Bw.harusi na mpambe wake wakiwa katika pozi
Bi.harusi na mpambe wake Catheline Nyoni katika pozi  
Bw.harusi na mpambe wake wakisakata rumba