Thursday, October 25, 2012

Serikali Mkoani Ruvuma imeapa kuwasaka kwaudi na uvumba wote wanaotaka kuvunja Amani


Na Steven Augustino,Tunduru                                                             
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amesema Serikali itahakikisha wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuanzia sasa wanarejea na kuanza kuishi maisha ya amani na utulivu kutokana na hatua kali zitakazo chukuliwa kwa watu ambao wamekuwa wakichochea vurugu,

Akizungumza katika mikutano tofauti mjini Tunduru alipokutana viongozi wa dini, watumishi wa halmashauri na baadaye katika  Mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Baraza la Idd mjini Tunduru.
Akifafanua taarifa hiyo Bw. Mwambungu alisema kuwa vitendo vya Kumpiga Shekh Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Alhaji Waziri Chilakwechi (75), Uchomaji wa Nguruwe, Magali na uhalibifu wa mali za wananchi wa Wilayani humo,

Ni uhalifu unaofanywa na wahuni ambao wanatumia mwamvuli wa Dini na kwa kujiita waislamu wenye msimamo mkali, hivyo kuanzi sasa watasakwa na kupelekwa katika mikono ya sheria.
Aidha Bw. Mwambungu akatumia nafasi hiyo kwa viongozi wa Serikari Mkoani Ruvuma kuwataka wachukue hatua za kisheria kwa wanaohatalisha amani na kuweka mikakati ya kuzuwia matukio yanayojitokeza katika maeneo yao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw Chande Nalicho akitoa taarifa za vitendo vya matukio yaliyosababisha tahaluki miongoni mwa jamii Wilayani Tunduru, Amesema kuwa Wilaya yake imejipanga kuhakikisha kuwa wahalifu hao wanachukuliwa hatua kulingana na makosa yao.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusdedit Nsimeki alisema kuwa tayali Jeshi hilo linawashikilia watu 6 ambao alidai kuwa taratibu za kuwapeleka mahakamani zinaendelea.
 Katika taarifa hiyo Kamanda Nsimeki aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shaibu Said(22), Rajab Abdalah (17),Bakali maloya (22) Rajab hasan (22),Ally  Kapopo (27) na Seleman Likoloma(20)ambao kwa pamoja walidaiwa kumshambulia Shekh Mkuu wa Wilaya hiyo.

Kufuatia hali hiyo kamanda Nsimeki pia akatumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kulisaidia jeshi hilo kutoa taarifa za wahalifu waliotekeleza matukio hayo na kusababisha tahaluki kwa jamii.

No comments:

Post a Comment