Tuesday, March 5, 2013

MKULIMA AUAWA NA TEMBO AKIJALIBU KUNUSULU MAZAO YAKE SHAMBANI


Mkazi wa Kijiji cha Nakatete katika kata ya Cheleweni Tarafa ya Mlingoti Mashariki Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma aliyea fahamika kwa jina la Rashidi Mohamed Moma (51) amefariki dunia baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na Tembo.

Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa Marehemu Moma  alikumbwa na mkasa huo  baada ya kukutana na tembo huyo ghafla wakati akikagua uhalibifu wa mazao uliofanywa na wanayama hao katika shamba lake lililopo inje kidogo ya kijiji hicho.

Wakiongea na mwandishi wa habari hizi baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa awali marehemu Moma aliwaaga kuwa anakwenda kuangalia mazao yake shambani baada ya Wanakijiji wenzake kushirika katika zoezi la kuwafukuza tembo hao ambao pia walivamia Kijijini hapo na kufanya uharibifu wa kubomoa nyumba kadhaa

Walisema katika tukio hilo la kushitukiza marehemu Moma  alijikuta akiwa mikononi mwa mnyama huyo ambaye hakuwa hana hata chembe moja ya huruma ambaye baada ya kumkamata klwa kutumia monga wake  alimrushwa juu na kukinga Pembe zake na kumtoboa toboa vibaya mbavuni na tumboni.
Diwani wa kata hiyo Bw. Adam Salum Mnandi akizungumzia hali na mwonekano wa mwili wa marehemu Moma alisema kuwa ama kwali mnyama huyo alimpania kumtoa uhai kwani pamoja na kumtoboa kwa kutumia pembe hizo pia Tembo huyo alimparua na kumkanyaga kanyaga na kuuvuruga kabisa mwili kiasi cha kufukia kutomtambua kabisa marehemu.
Akizungumzia tukio hilo kaimu wa kaimu afisa Wanyama pori wa Wilaya hiyo Bw. Charles shawa pamoja na kukiri kuwepo kwa tuikio hilo alisema kuwa tayari idara yake imepeleka asikari wenye silaha ili waende kuandaa mtego ambao utafanikisha kuuawa kwa mamba huyo.

Bw. Shawa aliendelea kueleza kuwa  matukio ya Tembo hao kuvamia na kuifanya uharibifu katika mashamba ya wakulima wa Wilaya hiyo yamekuwaa yakijitokeza mara kwa mara na kwamba kutokana na ahali hiyo idara yake imekuwa ikifanya kazi ya ziada kuwafukuza wanyama hao  ili wasiendelee kuharibu mazao ya watu.
Alisema pindi inapo bainika kuwa Tembo hao wanazidi kufanya mashambulizi ya kudhulu mwili ama kufanya mauaji kama ilivyo tokea idara hiyo pia imekuwa ikichukua hatua za kuwasakaa na kuwaua tembo hao haraka iwezekanavyo  ili asiendelee kusababisha madhara kwa watu wengine.
Akizungumzia hali na muonekano wa mwili wa marehemu huyo Mganga  katika hospitali hiyo Dkt….  Lusasi alisema kuwa Marehemu alifariki dunia kutokana na kutokwa na damu nyingi zilizo sababishwa na kutoboliowe matundu manne ubavuni na tumbino mwake.

Dkt.Vitaris  Lusasi aliendelea kueleza kuwa  sambamba na hali hiyo pia mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa umevurugika vibaya huku kishingo yake ikiwa imevunjika na kichwa kupasuka hali nayo onesha k,uiwa hata kama asingefariki katika eneo la tukio uwezekano wa kumsaidia kuokoa maisha yake usinge kuwepo.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusidedit Nsimeki amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi wa kina ili kujiridhisha chanzo cha kifo hicho.

No comments:

Post a Comment