Friday, October 4, 2013

KATIBU WA UWT TAIFA AMINA MAKILAGI AKAMILISHA ZIARA YA SIKU TATU WILAYANI TUNDURU.



Na shekhan mzaina

Katibu wa UWT Taifa MB.AMINA NASSORO MAKILAGI akiotekasalimiana na wananchi wa kjiji cha mchoteka  kata ya mchoteka.
 
Katibu wa jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi CCM na mmbunge wa viti maalum  AMINA NASSORO MAKILAGI amemaliza ziara iliyodumu kwa siku tatu katika wilaya ya Tunduru iliyoanza tarehe 1.10.2013 hadi tarehe 3.10.2013.


Katibu wa UWT Taifa MB.AMINA NASSORO MAKILAGI akihutubia wananchi wa kata ya namihungo wilayani Runduru mkoani Ruvuma.

Pichani wanakijiji cha nakapanya wakisikiliza hotuba ya Katibu wa UWT Taifa na  MB. viti maalum AMINA NASSORO MAKILAGI 

Wakati wa ziara yake wilayani humo yenye malengo mbalimbali ya  chama na serikali  amewataka wananchi hususani akinamama kuwapuuza baadhi ya wanasiasa  wanaochochea vurugu katika nchi yetu ya Tanzania kwani amani iliyopo hapa nchini haikupatikana hivihivi bali lipatikana kwa jasho na wananchi hawanabudi kuilinda amani hiyo,hata hivyo AMINA MAKILAGI amewasihi wanawake wa wilayahiyo kuwa mstari wa mbele kulinda amani nchini kwani wakati wa vurugu akinamama na watoto ndio waathirika wakubwa
.
Akizungumzia tatizo la maji ambalo ni tatizo sugu kwamaeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo  wilaya ya Tunduru  amesema serikali inamikakati kabambe ya kutatua tatizo hilo wilayani humo kwani katika bajeti ya mwaka 2013/2014 serikali imezamilia kupeleka huduma ya maji vijijini kwa kuongeza bajet ya wizara ya maji ili kujiondoa na utegemezi wa wahisani kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji  na kata za Nakapanya na Namihungo wilayani tunduru zitanufaika na mpango huo.

Kwa kutambua changamoto zilizopo katika sekta ya afya katibu huyo wa UWT taifa ameahidi kutoa msaada wa vitanda vine vya kujifungulia akinamama vyenye thamani ya shilingi milioni mbili na lakinane  kwa vituo vya afya vya Nakapanya na Mchoteka kwa mgawanyo sawa wa vitanda viwili kwa kila zaanati hizo.
 wanachama wapya wa chama cha mapinduzi CCM wakiapishwa wakati wa mkutano wa Katibu wa UWT Taifa MB.AMINA NASSORO MAKILAGI
Katika ziara yake hiyo wilaya humo UWT imeongeza wanachama wapya 127  katika kata tano za wilaya ya Tunduru huku wanachama sita kutoka chama cha wananchi CUF wamerudisha kadi na kujiunga na chama cha mapinduzi CCM.

Wednesday, May 8, 2013

MAJMBAZI YATEKA GARI NA KUPORA ABIRIA TUNDURU

Na Steven Augustino, Tunduru
WATU wawili waliofahamika kwa majina ya Ester gervas (60) na Gervas
Nipala (65) wamelazwa katika hospitali ya serikali ya Wilaya ya
Tunduru na wengine zaidi ya 30 walitibiwa na kuruhusiwa kuendelea na
safari yao baada ya kunusulika kifo katika tukio la gari waliyokuwa
wakisafilia kutekwa na majambazi.

Tukio lilo linalodaiwa kutekelezwa kundo la genge la majambazi hao
lilitokea katika eneo la Kijiji cha Shamba la Bibi katika tarafa ya
Nandembo Wilayani humo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya manusula wa tukio hilo
walisema kuwa mkasa huo uliwapata wakati wakisafiri kupitia basi mali
ya kampuni ya Komba Cochi ambalo hufanya safari zake kutoka Wilayani
Tunduru kwenda makao makuu ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea.

Hadija Isaa (30),Ester gervas (60) na Gervas Nipala (65) ambao
walikuwa miongoni mwa manusula hao walisema kuwa katika tukio hilo
maharamia hao walipiga na kuvunja kioo cha mbele cha gari hilo aina ya
Toyota DCM lenye namba za Usajiri T729 BRD na kutoa amri ya akuwataka
watoke nda ya gari na kuala chini huku wakiwa wamefumba macho.

Walisema baada ya abiria hao kutekeleza amri hiyo maharamia hao
waliwavamia na kuanza kuwapiga kwa kutumoa mapanga na magongo huku
wakiwasachi na kufanikiwa kuchukua kila walicho kiona kinafaa ikiwa ni
pamoja na kuwapora simu na fedha.

Akinzungumzia hali za majeruhi hao Mganga mfawidhi wa Hosptalai hiyo
Dkt. Joseph Ng’ombo alisema kuwa majeruhi hao wanaendelea vizuri
baada ya kupatima matibabu hayo na kwamba hata hivyo wabado wanhitaji
kuwa chini ya uangalizi wa maafisa tabibu kwa muda Fulani hadi hali
zao zitakapo imarika zaidi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusidedit Nsimeki amedhibitisha
kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa ingawa hadi sasa hakuna mtu
aliyetiwa mbaloni tayali jeshi la polisi kwa kushirikia na wasamaia
wema wamekwisha nasa mtandao wa majambazi hao na wamejipanga kwa ajili
ya kuanza kukabiliana nao kwa kuwakamata.

Alisema hata hivyo majamba hayo yalifanikiwa kupora simu za abilia
wachache na fedha tasilimu tsh.195,0000 na kwamba hali hiyo ilitokana
na majambazi hayo kurupushwa na kukimbizwa na Polisi ambao walikuwa
wakiongozwa na kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tunduru Bw. Amideus
Tesha ambao walienda kwa haraka baada ya kupatiwa taarifa za tukio
hilo kwa ajili ya kuwaokoa abiria hao.
Mwisho

Wednesday, April 3, 2013

TAASISI YA BENJAMINI WILLIAM MKAPA HIV/AIDS FOUNDATION YAENDELEA NA UHAMAMISISHAJI WA AJIRA KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI KWA WANAFUNZI WA VYUO VYA AFYA VILIVYOPO KATKA MANISPAA YA SONGEA MOANI RUVUMA.

Kaimu katibu tawala mkoa wa Ruvuma ndugu Severine Tossi kushoto akiwa na Mratibu wa kanda nyanda za juu kusini Bi Atuganile Jonas   katika unguzi wa uhamasishaji wa ajira katika sekta ya afya nchini kwa wanafunzi wa vyuo vya afya mkoani Ruvuma.

Katibu wa Afya manispaa ya Songea mjini Bw. George Mhina akifatilia kwa makini washa ya uhamasishaji wa ajira katika sekta ya afya nchini kwa wanafunzi wa vyuo vya afya mkoani Ruvuma
.................................................
Taasisi hii ya Benjamini William mkapa HIV/AIDS  imeendela kwa kuandaa maonyesho  ya uhamasishaji wa  ajira katika sekta ya afya nchini kwa wanafunzi na wahitimu wa vyuo vya afya katika manispaa ya songea.
Kwa hivi sasa sekta ya afya inakabiliwa na upungufu wa wataalam wa afya sehemu zote nchini lakini hali hii imeathiri zaidi sehemu za vijijini ambako ndiko waliko watanzania wengi.Kutokana na hali hiyo serikali nayo imeweza kujipanga ikishirikiana na wadau  mbalimbali ili kuweza kuinusuru hali ngumu ya kutokuwa na wataalamu wa kutosha.
Mikakati na miongozo mbalimbali inatekelezwa ikiwemo mpango Mkakati wa tatu wa Sekta ya Afya(Health Sector Sector Strategic Plan).Mipango iliyoainishwa  kwenye mikakati hii ni pamoja na kuweza kuhakikisha  kuwa wanapatikana wataalamu wa kutosha  ili waweze kuajiriwa na kutoa huduma zenye ubora kwa wananchi walio wengi. Hii ni pamoja na kuahamasisha wataalam wanaohitimu katika vyuo vya mafunzo waweze kuajiriwa katika sekta ya afya ili kuweza kuongeza idadi ya wataalamu wanaotoa huduma.
 Katika  hutuba iliyotolewa na Kaimu katibu tawala mkoa wa Ruvuma ndugu Severine Tossi katika chuo cha maafisa tabibu songea amesema malengo ya uhamasishaji huu ni kuelimisha juu ya nafasi za ajira katika  halmashauri za wilaya katika mkoa wa Ruvuma , Maboresho yaliyofanyika katika sekta ya afya na maslahi ya mfumo wa utunzaji, upatikanaji na ubadilishaji wa taarifa za wahitimu kati ya vyuo na waajiri (wizara husika na Halmashauri).
“ Ninaomba niwaase wanavyuo kuwa serikali inajitahidi kuboresha maslahi ya watumishi wake wote pamoja na wa sekta ya afya, Sisi ni mashuhuda  na tumeona  ni jinsi gani basi ajira katika sekta ya afya imeongezeka  mwaka hadi mwaka, pia imeendelea kutambua kada ambazo hapo awali hazikuwepo . Hii ni ishara kuwa serikali inajali na hivyo mna kila sababu za kukata shauri la kujiunga na sekta ya  afya”
Nae Atuganile Jonas ambaye ni Mratibu wa kanda nyanda za juu kusini amesema mbali na zoezi la uhamasishaji wa ajira katika halmashauri za mikoa mbalimbali hapa nchini Tanzania pia wameajili wa tumishi wa afya amabo wamepelekwa kwenye halmashauri mbalimabali “watumishi hao wapo chini ya taasisi kwa mkataba maalumu baada ya hapo halmashauri husika uwauwisha katika ajira ya serikali na kuwa watumishi wa umma”

Atuganile ameongezea kwa kusema taasisi hii ya Benjamini William mkapa HIV/AIDS Foundation inamradi wa ujenzi wa nyumba katika halmashauri sabani  katika mradi huo halimashauri moja hujengewa nyumba kumi mpaka sasa mkoani mtwara na lindi tayali wameshakamilisha na kukabidhi  nyumba hizo.
 Na kwa mkoa wa  Rukwa na Katavi nyumba zimeshakamlika bado makabidhiano na kwa upandea wa mkoa wa Ruvuma halmashsuri nne zitajengewa nyumba kumi kwa kila halmashaur moja ,nakati ya halmashauri hizo ni mbinga , namtumbo. Tunduru,songea vijijin,
Vilevile taasisi ya Benjamini William mkapa HIV/AIDS  Wanaufadhiri wa wanafunzi ambao wanaoenda kusoma katika vyuo vya afya kwa wale ambao wamefauru kwa kiwango lakini hawana uwezo kutokana na hali zao za kimaisha , Hadi sasa wanafunzi 150 wapo vyuooni kutokana na taasisi hii imeingia mkataba na halmasharu pamoja na wanafunzi kwa kuwapa msaada wa kuwaghalamikia masomo na baada ya kumaliza masomo yao watarudi katika halmashauri zao na kufanya kazi .

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA SIKU TATU WA MWAKA KUHUSU TAFITI ZA SERA NA MAENDELEO WA REPOA DAR

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa mkutano wakati akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi, wakati akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, akichangia wakati wa mkutano mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakiwa ukumbini humo wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Kunduchi Beach, kufungua ramsi mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, baada ya kuufungua mkutano huo ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa siku tatu wa mwaka kuhusu Tafiti za sera na Maendeleo wa Repoa, baada ya kuufungua mkutano hio, ulioanza leo April 3, 2013 katika Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Friday, March 8, 2013

MKUU WA MKOA WA RUVUMA SAID MWAMBUNGU ATOA ONYO KWA WALE WANAOUZA MAZAO YAO BILA KUSHIRIKISHA WAKE ZAO.



Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwangu akizungumza katika siku ya wanawake duniani

Mkuu wa Wialaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti akitambusha viongozi aliofatana nao
Mwenyekiti wa kamati ya wafanyakazi wanawake wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) Taifa dokta ANGELINA SANIKE akijitambulisha .

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akitoa zawadi ya sale ya shule, madaftali na sabuni kwa mtoto yatima ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akitoa zawadi ya sale ya shule, madaftali na sabuni kwa mtoto yatima ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari


 Kikundi cha ngoma ya asili kikitoa burudani ya (Ngoma ya Lizombe)
............................................................


Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia  iliyiadhimishwa kimkoa  katika kijiji cha Lusonga Wilaya ya Songea.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAIDI MWAMBUNGU amekemea vikali vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya wanawake katika mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha lusonga wilaya ya Songea hapo jana MWAMBUNGU amesema ni marufuku wanaume kuuza mazao yao bila kushirikisha wake zao. Na kwawale  wanaotenda hivo watachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa ni moja wapo ya ukatili dhidi ya wanawakePia  amesema serikali inafanya juhudi ya kutokomeza vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya wanawake.

Akisoma risala katika maadhimsho ya siku ya wanawake iliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Lusonga wilaya ya Songea mkoani Ruvuma afisa maendeleo ya jamii wa wilaya WENISARIA SWAI amesema kuwa katika mkoa wa Ruvuma wananawake ndio wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula na biashara lakini hawashirikishwi katika kutoa maamuzi.

Amesema wanawake wengi katika familia wananyimwahaki ya kushirikikatika kutoa maamuziya mgawanyo wa mapato yanayopatikana ingawa wao ndio wazalishaji na watendaji kazi wakubwa.Aidha shughuli nyingi zinazofanywa na wanaake hazina ujira hali inayosababisha ndoa kukosa malezi mema hatimaye watoto na vijana kuondoka nyumbani na kujiingiza katika makundi ya ombaomba mitani.

Naye mwenyekiti wa kamati ya wafanyakazi wanawake wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (talgwu) taifa dokta ANGELINA SANIKE ametoa wito kwa jamii kuelimsha watoto kike ili kuondokana na mfumo dume .


Wednesday, March 6, 2013

MKUU WA MKOA WA RUKWA AKAGUA MIRADI YA USIMAMIZI WA ZIWA TANGANYIKA (PRODAP) KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SUMBAWANGA


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwa na msafara wake wakikagua ujenzi unaoendelea wa daharia (bweni) katika shule ya sekondari Kasanga. Mradi huo ni sehemu ya miradi inayofadhiliwa na mradi wa usimazi wa ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na miradi mingine ya ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Muzi na ujenzi wa wadi ya kujifungulia kinamama kijiji cha Samazi. Miradi yote hiyo itawanufaisha wakazi wa mwambao wa ziwa Tanganyika na inagharimu zaidi ya shilingi milioni 150.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Samazi mwambao na ziwa Tanganika alipofika kukagua ujenzi wa wadi ya kujifungulia kinamama katika kijiji hicho. Mkuu huyo wa Mkoa alimuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuwafuatilia kwa karibu wahandisi wanaojenga miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati. Aliwaasa pia wananchi kuzingatia uzazi wa mpango katika kuboresha maisha yao pamoja na kuwaendelezea watoto wao kielimu tofauti na hali ilivyo hivi sasa ambapo muamko wa elimu Mkoani Rukwa upo chini. Aliwataka pia kuboresha hali ya ulinzi katika maeneo yao ya mipakani kwa kutokuwakaribisha wageni bila kuwa na taarifa zao za kutosha.
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na msafara wake wakikagua ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya Msingi Muzi yaliyowekwa jiwe la msingi na Naibu Waziri wa TAMISEMI Aggrey Mwanri ambayo mpaka kukamilika kwake yatagharimu zaidi ya shilingi Milioni 50. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Muzi iliyopo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika Mkoani Rukwa baada ya kukagua ujenzi unaoendelea wa madara yanayofadhiliwa na mradi wa usimamizi wa ziwa Tanganyika mradi ambao upo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira. Aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwaahidi kuwapa ushirikiano wale watakaofaulu vizuri na kukosa uwezo wa kujiendeleza.
 
Sehemu ya fukwe ya Ziwa Tanganyika katika kijiji cha Samazi Mkoani Rukwa ambapo mradi wa usimamizi wa ziwa Tanganyika unatekeleza mradi wa ujenzi wa wadi ya kinamama kwa ajili ya kujifungulia katika Zahanati ya kijiji hicho.

WANAWAKE WAHIMIZWA KUACHA UKATILI WA KUUA VICHANGA


 Wakati umoja wa akina mama wa Makanisa ya kikristo Duniani yakikemea ukatili wa Kutupa watoto ambao umekuwa ukifanywa na wanawake Mkazi wa Kijiji cha Mchangani mjini Tunduru Mkoani Ruvuma aliyefahamika  kwa jina la Sikudhani Ajali amefariki dunia wakati akijaribu kutoa mimba.

Akiongea kupita mahubiri katika maadhimisho ya maombi ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika Parokia ya kanisa la Mtakatifu  maria imakrata Jimbo la TUNDURU masasi  mhubiri kutoka kanisa la KKKT  Jane Ndonde alioneshwa kukerwa kuwepo kwa taarifa nyingi za matukio hayo zinaelezea ukatili mkubwa ukiwemo wa kuua,kutelekeza ,kutumbukiza watoto vyooni na hata kuwazika watoto wao wakiwa wazima kwea visingizio vyo kutelekezwa na waume zao.

Kuhusu tukio jipya la kujiua kwa marehemu Sikudhani ambaye alidaiwa kujiua kwea sababu ya kutelekezwa na mcumba wake ambaye alikuwa akiishi nae Jijini Dar es salaam muhubiri huyo alidai kuwa Marehemu ambaye amewahi kuwa na watoto zaidi ya 3 kabla ya ujauzito huo alichuku uamuzi huo bila kufikiria na mndiyo maana mungu amemlipa kwa mtindo huo.

Kufuatia hali hiyo Ndonde amabye alinukuu maandiko matakatifu  akatumia nafasi hiyo kuwakumbusha wanawake wa Tanzania na Dunia nzima kutimiza wajibu wao na kukemia vitendo vyote viovu kupitia mwongozo waliopewa kutokaa Umoja wa Makanisa Duniani  kupitia kauli mbiu ya mwaka 2013 inayo sema kuwa   “NILIKUWA MGENI MKANIKARIBISHA” Mathayo sura ya 25.35C. 

Aidha katika hutuba huyi pia Bi. Ndonde aliwaasa wakrsto nchini kutakasa roho zao na kutokubali kuingia katika mkumbo wa mapigano ya kidini yanayo lazimishwa kufanywa na waumini wa dini zingine kufuatia daliliza za mapigano hayo kuanza kutokea katika Mikoa ya Kagera na Ruvuma Wilayani tunduru na Zanziobar.  

Akiongea kwa niaba ya wanafamilia juu ya tukio hilo Diwani wa Kata ya Mchangani Bw.Adam Madina alisema kuwa taarfa zinaonesha kuwa Marehemu alichukua uamuzi huo kufuatia msongo wa mawazo uliosababishwa na tukio la mwanaume huyo kuikataa mimba hiyo
Bw.Madina aliendelea kueleza kuwa mbali na wanafamilia kumsihi asiitoe mimba hiyo kwa siku kadhaa alizoishi Mjini hapa baada ya kukimbia ugomvi huo kwa mchumba wake huyo lakini alionekana kuendelea na msimamo wake wa kuitoa mimba hiyo na kuishia kukubwa na umauti.

 Wakizungumzia tukio hilo miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa baada yamarehemu kukatazwa kufanya jaribio hilo marehemu aliamua kumeza lundo la vidonge akiwa chooni ambako hata baada ya kuziwa hakuweza kupata msaada wa kuokoa maisha yake kiraahisi na kusababisha kifo chake.

Awali akisoma risala ya maadhimisho hayo Mwenyekiti wa jumuiya inayo inayo waunganisha akina mama wa kikristo Wilayani Tunduru  Rehema Ligombaji alisema kuwa maombi hayo yamefanikishwa na waumini kutopka katika makanisa ya Romani katholiki,Angalikana,Bibilia,Rutherani,Moraviani na Kanisa la Upendo Kriosto masihi.

Mwisho

Tuesday, March 5, 2013

MKULIMA AUAWA NA TEMBO AKIJALIBU KUNUSULU MAZAO YAKE SHAMBANI


Mkazi wa Kijiji cha Nakatete katika kata ya Cheleweni Tarafa ya Mlingoti Mashariki Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma aliyea fahamika kwa jina la Rashidi Mohamed Moma (51) amefariki dunia baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na Tembo.

Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa Marehemu Moma  alikumbwa na mkasa huo  baada ya kukutana na tembo huyo ghafla wakati akikagua uhalibifu wa mazao uliofanywa na wanayama hao katika shamba lake lililopo inje kidogo ya kijiji hicho.

Wakiongea na mwandishi wa habari hizi baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa awali marehemu Moma aliwaaga kuwa anakwenda kuangalia mazao yake shambani baada ya Wanakijiji wenzake kushirika katika zoezi la kuwafukuza tembo hao ambao pia walivamia Kijijini hapo na kufanya uharibifu wa kubomoa nyumba kadhaa

Walisema katika tukio hilo la kushitukiza marehemu Moma  alijikuta akiwa mikononi mwa mnyama huyo ambaye hakuwa hana hata chembe moja ya huruma ambaye baada ya kumkamata klwa kutumia monga wake  alimrushwa juu na kukinga Pembe zake na kumtoboa toboa vibaya mbavuni na tumboni.
Diwani wa kata hiyo Bw. Adam Salum Mnandi akizungumzia hali na mwonekano wa mwili wa marehemu Moma alisema kuwa ama kwali mnyama huyo alimpania kumtoa uhai kwani pamoja na kumtoboa kwa kutumia pembe hizo pia Tembo huyo alimparua na kumkanyaga kanyaga na kuuvuruga kabisa mwili kiasi cha kufukia kutomtambua kabisa marehemu.
Akizungumzia tukio hilo kaimu wa kaimu afisa Wanyama pori wa Wilaya hiyo Bw. Charles shawa pamoja na kukiri kuwepo kwa tuikio hilo alisema kuwa tayari idara yake imepeleka asikari wenye silaha ili waende kuandaa mtego ambao utafanikisha kuuawa kwa mamba huyo.

Bw. Shawa aliendelea kueleza kuwa  matukio ya Tembo hao kuvamia na kuifanya uharibifu katika mashamba ya wakulima wa Wilaya hiyo yamekuwaa yakijitokeza mara kwa mara na kwamba kutokana na ahali hiyo idara yake imekuwa ikifanya kazi ya ziada kuwafukuza wanyama hao  ili wasiendelee kuharibu mazao ya watu.
Alisema pindi inapo bainika kuwa Tembo hao wanazidi kufanya mashambulizi ya kudhulu mwili ama kufanya mauaji kama ilivyo tokea idara hiyo pia imekuwa ikichukua hatua za kuwasakaa na kuwaua tembo hao haraka iwezekanavyo  ili asiendelee kusababisha madhara kwa watu wengine.
Akizungumzia hali na muonekano wa mwili wa marehemu huyo Mganga  katika hospitali hiyo Dkt….  Lusasi alisema kuwa Marehemu alifariki dunia kutokana na kutokwa na damu nyingi zilizo sababishwa na kutoboliowe matundu manne ubavuni na tumbino mwake.

Dkt.Vitaris  Lusasi aliendelea kueleza kuwa  sambamba na hali hiyo pia mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa umevurugika vibaya huku kishingo yake ikiwa imevunjika na kichwa kupasuka hali nayo onesha k,uiwa hata kama asingefariki katika eneo la tukio uwezekano wa kumsaidia kuokoa maisha yake usinge kuwepo.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusidedit Nsimeki amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi wa kina ili kujiridhisha chanzo cha kifo hicho.

WAKALA wa Nishati vijijini kupitia wadhamini wa Rural Energy Agency (REA) kukijengea kikosi cha JKT Mlale mtambo wa kuzalisha umeme wa BIYOGESI ambao utakagharimu kiasi cha shilingi milioni 123



Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph Mkirikiti akisisitiza jambo katika ufunguzi wa mafunzo katika kikosi cha JKT Mlale

Meneja wa mafunzo na ujengaji uwezo Grace Mathew akitoa maelezo mbele ya mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti.
  Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemoakitoa maelekezo kuhusu mtambo utakao wekwa katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka mtambo.
  Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemoakitoa maelekezo kuhusu mtambo utakao wekwa katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka mtambo.
Shimo hili ni lamtambo utakao wekwa
 ......................................................................................
 WAKALA wa Nishati vijijini kwa kupitia wadhamini wa Rural Energy Agency (REA)wametoa mafunzo ya utengenezaji wa mitambo ya umeme ya Biyogesi kwa kikosi cha JKT MLALE ,842KJ kilichopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma pamoja na kuwajengea mtambo wa umeme huo kikosini hapo  utakao garimu milioni 123 ,ili kufanikisha kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo na uharibifu wa mazingira.

  Akiongea jana meneja wa mafunzo na ujengaji uwezo Grace Mathew mbele ya mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia sana katika hali ya kukambiliana na changamoto za ukosefu wa wa Nishati ya umeme pamoja na uharibifu wa mazingira kwa kukata miti kwa ajili ya mkaa na kuni.
 
  Methew alisema kuwa wameamua kutoa mafunzo kikosini hapo kwa kuwa watu wa sekta hizo za JKT ndio wenye uzalendo mkubwa wa kutoa elimu hiyo kwa vijana mbalimbali hasa waliyopo mafunzoni kwenye vikosi hivyo na kuwa vijana hao pia wataenda kutoa elimu hiyo kwa wananchi wengine ikiwemo na kuwatengezea mitambo hiyo ambayo garama yake ni nafuu.

 “Nasema ni garama nafuu kwa kuwa kunamitambo midogo kulingana na uhitaji wa mwanachi mwenyewe anavyohitaji matumizi yake ya umeme huo na kuwa sasa ni zamu ya watu wa vijini kunifaika na hiyo mitambo ya biyogesi na kuachana na tabia ya kuona umeme wanapata watu wa mijini tuu”alisema meneja huyo.
  
  “Vijijini siku zote walikuwa wakitoa michango yao  kwa serikali kupitia  ulipaji  kodi ya vitu mbalimbali ndani mwake kukiwemo na suala la umeme sasa ni wakati wa kuwatambua na wao kuwa wapate umeme ambao hawata kuwa na garama ya kuwajibika TANESCO kama ilivyo kwa umeme unaotumika mijini”alisema.
     
  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti akisoma hotuba yake wakati akifungua mafunzo hayo alisema kuwa ni vyema sasa suala hilo la umeme wa biyogesi lizingatiwe kwa umakini ili kuondokana na uharibifu unaofanywa katika misitu mbalimbali hapa nchini.
    
   Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa zoezi hilo likifanikiwa litasaidia sana hata kwa vijana ambao kwa sasa wamekosa ajira hivyo kwa kufanya kazi hiyo ya ujenzi wa mitambo hiyo kwao itakuwa ni ajira tosha  na hatimaye watainua uchumi ndani ya Taifa pamoja na uchumi wao .
       
   “Naomba niseme kwa moyo wa dhati umeme wa mtindo huo nimeshauona na nimeona manufaa yake hivyo ningeliomba hata kwa wabunge wetu wawapo mbungeni kuliongelea suala la umeme wa biyogesi kwa wananchi kwa kuwa ni sehemu ya ilani ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi CCM”alisema kuwa kila mwanachi anahaki ya kutumia Nishati hiyo.
          
  “Leo kikosi hiki cha JKT MLALE mnajengewa mtambo wa uzalishaji wa umeme wa biyogesi wenye thamani ya milioni 123 utakao kamilika ndani ya miezi miwili na kupata umeme ambao hauna ugovi na shirika la TANESCO je mngesubiri umeme wa gridi ya Taifa mgepata leo “alisema mkuu huyo wa wilaya.
       
 Alisema kuwa sina maana kuwa umeme wa gridi ya Taifa usifike Songea bali nasema wakati umeme huo unasubiriwa sisi tuwe na umeme mbadala ambao hauna garama ya kutumia na kwamba umeme huo hauna kuweka manguzo bali ni wewe na Nyumba yako.
      
  Naye Meja mkuu wa kikosi hicho Thomas Mpuku alipongeza jidihada zilizofanywa na watu wa Wakala wa Nishati vijijini kwa ubunifu wao mkubwa na kuendesha mafunzo hayo katika kikosi chake na kuwa yeye atahakikisha elimu hiyo inaendelezwa na wengine .

   Aidha Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemo ambaye anasimamia ujenzi wa mtambo huo katika kikosi cha JKT MLALE alisema kuwa ukifanikiwa kuwa na mtambo wa biyogesi kazi yako kubwa ni kutumbukiza taka unazo zizalisha kwenye mtambo huo ili kuendelea kupata umeme.

 Hata hivyo alisema kuwa wamesha pita katika maeneo  mbalimbali kutoa elimu hiyo na kujenga mitambo hiyo na sasa tayari wananufaika nayo na pia wataendelea kwenda katika maeneo mengine kutoa elimu hiyo.
    
Picha na habari www.demashonews.blogspot.com

Saturday, February 23, 2013

TBC YATOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI SHULE YA UHURU MCHANGANYIKO

001Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (katikat) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana kuhusu maktaba hiyo wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam leo. Wengine ni Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mang’enya (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa tatu kushoto) na wafanyakazi wengine wa Vita Foam, TBC na walimu wa shule hiyo.
Shirika la Utangazaji nchini (TBC) pamoja na Kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited, leo wamekabidhi msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 3 kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam. Msaada huo ni sehemu ya marejesho ya faida inayoipata kwa jamii (CSR).
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana amesema Jamii inayo wajibu wa kusaidia makundi ya watoto wenye ulemavu nchini ili kuwapa faraja na wajione nao ni sehemu ya jamii.
003Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto) moja ya nyenzo zinazotumiwa na
wanafunzi walemavu kuandikia wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam jana.
004Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto) moja ya kompyuta zinazotumiwa na wanafunzi walemavu kusomea wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya
sh milioni 3, Dar es Salaam jana. 
006
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi moja ya mashine inayotumiwa na watoto walemavu wa macho kuandikia kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mang’enya wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam jana.
007
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi sehemu ya magodoro 100 yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa Mratibu wa Elimu Kata ya Gerezani, Seraphina Mdamu kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi walemavu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited walipokwenda kutoa msaada huo shuleni hapo, Dar es Salaam jana. Wengine ni Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mang’enya na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa pili kulia).

Tuesday, February 19, 2013

KAMPUNI YA GAME FRONTIERS OF TANZANIA WAMEFANIKIWA KUKAMATA NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA MILION MIAMBILI - NAMTUMBO.


Hawa ni wafanyakazi wa Game frontiers of Tanzania wakiwa wamebeba pembe za ndovu
Pembe za ndovu, Risasi na Silaha zilizokamatwa

Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni ya Game Frontiers of Tanzania akifanya mahojiano na Bw. Gerson Msigwa ambaye ni mtangazaji wa TBC.


Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA kwa kushirikiana askari wanyamapori wa Selou na Askari wa vijiji vinavyozunguka pori la Akiba la Selou wamefanikiwa kukamata meno ya tembo 15 yenye thamani ya milion miambili, Risasi 9, Bunduki moja aina ya RIFFLE 458 na Gobole moja ambavyo hutumika kuulia wanyama .

Doria hiyo imechukua takribani siku tatu katika pori la Akiba la Selou ikiwa ni sehemu ya kuwatafuta majangili wanaofanya mauaji ya wanyamapori katika pori hilo,
Akizungumza na mwandishi wetu Bw. Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni hiyo ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA, Amesema kuwa hiyo ni kujituma kutokana na motisha ya fedha anayoitoa mwezeshaji wa kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA ndio chachu ya mafanikio ya kukamata meno,bunduki na risasi.

 Akiendelea kuzungumzia tukio hilo Bw. Mohamed Mpapa amesmea baada ya majangili kuwaona Game Frontiers Tanzania wakiwa katika doria ndani ya pori hilo huku wakiwa wamekamilika kimapigano majangili hao waliweza kukimbia na kuacha nyara hizo baada ya kuona nguvu yao ni ndogo katika kupambana na kundi la doria.

Ameongezea kwa kusema Kampuni yake imefurahishwa na mafanikio na ushirikiano uliopo kati yao, Serikali na wanavijiji kukabiliana na ujangili unaoendelea kuwamaliza tembo katika Pori la Akiba la Selou pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kuwafichua majangili.

Nae Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la Selou Bw. Bernald Lijaji amesema Pembe zilizokamatwa ni 15 pamoja na Bunduki aina ya RIFLE 458,Gobole moja na Risasi 9 aina ya 458 vimekamatwa katika Doria iliyofadhiriwa na Mwekezaji wa Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA