Wakati umoja wa akina mama wa Makanisa ya kikristo Duniani yakikemea ukatili wa Kutupa watoto ambao umekuwa ukifanywa na wanawake Mkazi wa Kijiji cha Mchangani mjini Tunduru Mkoani Ruvuma aliyefahamika kwa jina la Sikudhani Ajali amefariki dunia wakati akijaribu kutoa mimba.
Akiongea kupita
mahubiri katika maadhimisho ya maombi ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika
katika Parokia ya kanisa la Mtakatifu maria imakrata Jimbo la
TUNDURU masasi mhubiri kutoka kanisa la KKKT Jane Ndonde
alioneshwa kukerwa kuwepo kwa taarifa nyingi za matukio hayo zinaelezea ukatili
mkubwa ukiwemo wa kuua,kutelekeza ,kutumbukiza watoto vyooni na hata kuwazika
watoto wao wakiwa wazima kwea visingizio vyo kutelekezwa na waume zao.
Kuhusu tukio jipya
la kujiua kwa marehemu Sikudhani ambaye alidaiwa kujiua kwea sababu ya
kutelekezwa na mcumba wake ambaye alikuwa akiishi nae Jijini Dar es salaam
muhubiri huyo alidai kuwa Marehemu ambaye amewahi kuwa na watoto zaidi ya 3
kabla ya ujauzito huo alichuku uamuzi huo bila kufikiria na mndiyo maana mungu
amemlipa kwa mtindo huo.
Kufuatia hali hiyo
Ndonde amabye alinukuu maandiko matakatifu akatumia nafasi hiyo kuwakumbusha
wanawake wa Tanzania na Dunia nzima kutimiza wajibu wao na kukemia vitendo
vyote viovu kupitia mwongozo waliopewa kutokaa Umoja wa Makanisa
Duniani kupitia kauli mbiu ya mwaka 2013 inayo sema kuwa “NILIKUWA
MGENI MKANIKARIBISHA” Mathayo sura ya 25.35C.
Aidha katika hutuba
huyi pia Bi. Ndonde aliwaasa wakrsto nchini kutakasa roho zao na kutokubali
kuingia katika mkumbo wa mapigano ya kidini yanayo lazimishwa kufanywa na
waumini wa dini zingine kufuatia daliliza za mapigano hayo kuanza kutokea katika
Mikoa ya Kagera na Ruvuma Wilayani tunduru na Zanziobar.
Akiongea kwa niaba
ya wanafamilia juu ya tukio hilo Diwani wa Kata ya Mchangani
Bw.Adam Madina alisema kuwa taarfa zinaonesha kuwa Marehemu alichukua
uamuzi huo kufuatia msongo wa mawazo uliosababishwa na tukio la mwanaume huyo
kuikataa mimba hiyo
Bw.Madina
aliendelea kueleza kuwa mbali na wanafamilia kumsihi asiitoe mimba hiyo kwa
siku kadhaa alizoishi Mjini hapa baada ya kukimbia ugomvi huo kwa mchumba wake
huyo lakini alionekana kuendelea na msimamo wake wa kuitoa mimba hiyo na
kuishia kukubwa na umauti.
Wakizungumzia
tukio hilo miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa baada yamarehemu
kukatazwa kufanya jaribio hilo marehemu aliamua kumeza lundo la vidonge akiwa
chooni ambako hata baada ya kuziwa hakuweza kupata msaada wa kuokoa maisha yake
kiraahisi na kusababisha kifo chake.
Awali akisoma
risala ya maadhimisho hayo Mwenyekiti wa jumuiya inayo inayo waunganisha akina
mama wa kikristo Wilayani Tunduru Rehema Ligombaji alisema kuwa
maombi hayo yamefanikishwa na waumini kutopka katika makanisa ya Romani
katholiki,Angalikana,Bibilia,Rutherani,Moraviani na Kanisa la Upendo Kriosto
masihi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment