Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph Mkirikiti akisisitiza jambo katika ufunguzi wa mafunzo katika kikosi cha JKT Mlale
Meneja wa mafunzo na ujengaji uwezo Grace Mathew akitoa maelezo mbele ya mkuu wa wilaya ya
Songea Joseph Mkilikiti.
Injinia
wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemoakitoa maelekezo kuhusu mtambo utakao wekwa katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka mtambo.
Injinia
wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemoakitoa maelekezo kuhusu mtambo utakao wekwa katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka mtambo.
Shimo hili ni lamtambo utakao wekwa
......................................................................................
WAKALA wa
Nishati vijijini kwa kupitia wadhamini wa Rural Energy Agency (REA)wametoa
mafunzo ya utengenezaji wa mitambo ya umeme ya Biyogesi kwa kikosi cha JKT
MLALE ,842KJ kilichopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma pamoja na kuwajengea
mtambo wa umeme huo kikosini hapo utakao garimu milioni 123 ,ili
kufanikisha kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo na uharibifu wa mazingira.
Akiongea jana
meneja wa mafunzo na ujengaji uwezo Grace Mathew mbele ya mkuu wa wilaya ya
Songea Joseph Mkilikiti alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia sana katika hali
ya kukambiliana na changamoto za ukosefu wa wa Nishati ya umeme pamoja na
uharibifu wa mazingira kwa kukata miti kwa ajili ya mkaa na kuni.
Methew alisema kuwa
wameamua kutoa mafunzo kikosini hapo kwa kuwa watu wa sekta hizo za JKT ndio
wenye uzalendo mkubwa wa kutoa elimu hiyo kwa vijana mbalimbali hasa waliyopo
mafunzoni kwenye vikosi hivyo na kuwa vijana hao pia wataenda kutoa elimu hiyo
kwa wananchi wengine ikiwemo na kuwatengezea mitambo hiyo ambayo garama yake ni
nafuu.
“Nasema ni garama
nafuu kwa kuwa kunamitambo midogo kulingana na uhitaji wa mwanachi mwenyewe
anavyohitaji matumizi yake ya umeme huo na kuwa sasa ni zamu ya watu wa vijini
kunifaika na hiyo mitambo ya biyogesi na kuachana na tabia ya kuona umeme
wanapata watu wa mijini tuu”alisema meneja huyo.
“Vijijini siku zote
walikuwa wakitoa michango yao kwa serikali kupitia ulipaji
kodi ya vitu mbalimbali ndani mwake kukiwemo na suala la umeme sasa ni wakati
wa kuwatambua na wao kuwa wapate umeme ambao hawata kuwa na garama ya
kuwajibika TANESCO kama ilivyo kwa umeme unaotumika mijini”alisema.
Kwa upande wake
mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti akisoma hotuba yake wakati akifungua
mafunzo hayo alisema kuwa ni vyema sasa suala hilo la umeme wa biyogesi
lizingatiwe kwa umakini ili kuondokana na uharibifu unaofanywa katika misitu
mbalimbali hapa nchini.
Mkuu huyo wa
wilaya alisema kuwa zoezi hilo likifanikiwa litasaidia sana hata kwa vijana
ambao kwa sasa wamekosa ajira hivyo kwa kufanya kazi hiyo ya ujenzi wa mitambo
hiyo kwao itakuwa ni ajira tosha na hatimaye watainua uchumi ndani ya
Taifa pamoja na uchumi wao .
“Naomba
niseme kwa moyo wa dhati umeme wa mtindo huo nimeshauona na nimeona manufaa
yake hivyo ningeliomba hata kwa wabunge wetu wawapo mbungeni kuliongelea suala
la umeme wa biyogesi kwa wananchi kwa kuwa ni sehemu ya ilani ya utekelezaji wa
chama cha Mapinduzi CCM”alisema kuwa kila mwanachi anahaki ya kutumia Nishati
hiyo.
“Leo kikosi hiki
cha JKT MLALE mnajengewa mtambo wa uzalishaji wa umeme wa biyogesi wenye
thamani ya milioni 123 utakao kamilika ndani ya miezi miwili na kupata umeme
ambao hauna ugovi na shirika la TANESCO je mngesubiri umeme wa gridi ya Taifa
mgepata leo “alisema mkuu huyo wa wilaya.
Alisema kuwa sina
maana kuwa umeme wa gridi ya Taifa usifike Songea bali nasema wakati umeme huo
unasubiriwa sisi tuwe na umeme mbadala ambao hauna garama ya kutumia na kwamba
umeme huo hauna kuweka manguzo bali ni wewe na Nyumba yako.
Naye Meja mkuu wa
kikosi hicho Thomas Mpuku alipongeza jidihada zilizofanywa na watu wa Wakala wa
Nishati vijijini kwa ubunifu wao mkubwa na kuendesha mafunzo hayo katika kikosi
chake na kuwa yeye atahakikisha elimu hiyo inaendelezwa na wengine .
Aidha Injinia
wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemo ambaye anasimamia ujenzi wa mtambo
huo katika kikosi cha JKT MLALE alisema kuwa ukifanikiwa kuwa na mtambo wa
biyogesi kazi yako kubwa ni kutumbukiza taka unazo zizalisha kwenye mtambo huo
ili kuendelea kupata umeme.
Hata hivyo alisema
kuwa wamesha pita katika maeneo mbalimbali kutoa elimu hiyo na kujenga
mitambo hiyo na sasa tayari wananufaika nayo na pia wataendelea kwenda katika
maeneo mengine kutoa elimu hiyo.
Picha na habari www.demashonews.blogspot.com
No comments:
Post a Comment