Mkazi wa Kijiji cha Nakatete katika kata ya Cheleweni Tarafa ya Mlingoti Mashariki Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma aliyea fahamika kwa jina la Rashidi Mohamed Moma (51) amefariki dunia baada ya kuvamiwa na kushambuliwa na Tembo.
Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa Marehemu Moma alikumbwa na mkasa huo baada
ya kukutana na tembo huyo ghafla wakati akikagua uhalibifu wa mazao
uliofanywa na wanayama hao katika shamba lake lililopo inje kidogo ya
kijiji hicho.
Wakiongea
na mwandishi wa habari hizi baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo walisema
kuwa awali marehemu Moma aliwaaga kuwa anakwenda kuangalia mazao yake
shambani baada ya Wanakijiji wenzake kushirika katika zoezi la
kuwafukuza tembo hao ambao pia walivamia Kijijini hapo na kufanya
uharibifu wa kubomoa nyumba kadhaa
Walisema katika tukio hilo la kushitukiza marehemu Moma alijikuta
akiwa mikononi mwa mnyama huyo ambaye hakuwa hana hata chembe moja ya
huruma ambaye baada ya kumkamata klwa kutumia monga wake alimrushwa juu na kukinga Pembe zake na kumtoboa toboa vibaya mbavuni na tumboni.
Diwani
wa kata hiyo Bw. Adam Salum Mnandi akizungumzia hali na mwonekano wa
mwili wa marehemu Moma alisema kuwa ama kwali mnyama huyo alimpania
kumtoa uhai kwani pamoja na kumtoboa kwa kutumia pembe hizo pia Tembo
huyo alimparua na kumkanyaga kanyaga na kuuvuruga kabisa mwili kiasi cha
kufukia kutomtambua kabisa marehemu.
Akizungumzia
tukio hilo kaimu wa kaimu afisa Wanyama pori wa Wilaya hiyo Bw. Charles
shawa pamoja na kukiri kuwepo kwa tuikio hilo alisema kuwa tayari idara
yake imepeleka asikari wenye silaha ili waende kuandaa mtego ambao
utafanikisha kuuawa kwa mamba huyo.
Bw. Shawa aliendelea kueleza kuwa matukio
ya Tembo hao kuvamia na kuifanya uharibifu katika mashamba ya wakulima
wa Wilaya hiyo yamekuwaa yakijitokeza mara kwa mara na kwamba kutokana
na ahali hiyo idara yake imekuwa ikifanya kazi ya ziada kuwafukuza
wanyama hao ili wasiendelee kuharibu mazao ya watu.
Alisema
pindi inapo bainika kuwa Tembo hao wanazidi kufanya mashambulizi ya
kudhulu mwili ama kufanya mauaji kama ilivyo tokea idara hiyo pia
imekuwa ikichukua hatua za kuwasakaa na kuwaua tembo hao haraka
iwezekanavyo ili asiendelee kusababisha madhara kwa watu wengine.
Akizungumzia hali na muonekano wa mwili wa marehemu huyo Mganga katika hospitali hiyo Dkt…. Lusasi
alisema kuwa Marehemu alifariki dunia kutokana na kutokwa na damu
nyingi zilizo sababishwa na kutoboliowe matundu manne ubavuni na tumbino
mwake.
Dkt.Vitaris Lusasi aliendelea kueleza kuwa sambamba
na hali hiyo pia mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa umevurugika vibaya
huku kishingo yake ikiwa imevunjika na kichwa kupasuka hali nayo onesha
k,uiwa hata kama asingefariki katika eneo la tukio uwezekano wa
kumsaidia kuokoa maisha yake usinge kuwepo.
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deusidedit Nsimeki amedhibitisha kuwepo
kwa tukio hilo na kueleza kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi
wa kina ili kujiridhisha chanzo cha kifo hicho.
No comments:
Post a Comment