Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiwa na msafara wake wakikagua ujenzi
unaoendelea wa daharia (bweni) katika shule ya sekondari Kasanga. Mradi
huo ni sehemu ya miradi inayofadhiliwa na mradi wa usimazi wa ziwa
Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na
miradi mingine ya ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule
ya msingi Muzi na ujenzi wa wadi ya kujifungulia kinamama kijiji cha
Samazi. Miradi yote hiyo itawanufaisha wakazi wa mwambao wa ziwa
Tanganyika na inagharimu zaidi ya shilingi milioni 150.
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Samazi mwambao na ziwa
Tanganika alipofika kukagua ujenzi wa wadi ya kujifungulia kinamama
katika kijiji hicho. Mkuu huyo wa Mkoa alimuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kuwafuatilia kwa karibu wahandisi
wanaojenga miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati. Aliwaasa pia
wananchi kuzingatia uzazi wa mpango katika kuboresha maisha yao pamoja
na kuwaendelezea watoto wao kielimu tofauti na hali ilivyo hivi sasa
ambapo muamko wa elimu Mkoani Rukwa upo chini. Aliwataka pia kuboresha
hali ya ulinzi katika maeneo yao ya mipakani kwa kutokuwakaribisha
wageni bila kuwa na taarifa zao za kutosha.
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa na msafara wake wakikagua ujenzi wa madarasa matatu katika shule
ya Msingi Muzi yaliyowekwa jiwe la msingi na Naibu Waziri wa TAMISEMI
Aggrey Mwanri ambayo mpaka kukamilika kwake yatagharimu zaidi ya
shilingi Milioni 50.
Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na wanafunzi wa shule ya
msingi Muzi iliyopo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika Mkoani Rukwa baada ya
kukagua ujenzi unaoendelea wa madara yanayofadhiliwa na mradi wa
usimamizi wa ziwa Tanganyika mradi ambao upo chini ya Ofisi ya Makamu wa
Rais Mazingira. Aliwaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuwaahidi
kuwapa ushirikiano wale watakaofaulu vizuri na kukosa uwezo wa
kujiendeleza.
Sehemu ya fukwe ya
Ziwa Tanganyika katika kijiji cha Samazi Mkoani Rukwa ambapo mradi wa
usimamizi wa ziwa Tanganyika unatekeleza mradi wa ujenzi wa wadi ya
kinamama kwa ajili ya kujifungulia katika Zahanati ya kijiji hicho.
No comments:
Post a Comment