Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwangu akizungumza katika siku ya wanawake duniani
Mkuu wa Wialaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti akitambusha viongozi aliofatana nao
Mwenyekiti
wa kamati ya wafanyakazi wanawake wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa
(TALGWU) Taifa dokta ANGELINA SANIKE akijitambulisha .
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akitoa zawadi ya sale ya shule,
madaftali na sabuni kwa mtoto yatima ambaye ni mwanafunzi wa shule ya
msingi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akitoa zawadi ya sale ya shule,
madaftali na sabuni kwa mtoto yatima ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari
Kikundi cha ngoma ya asili kikitoa burudani ya (Ngoma ya Lizombe)
............................................................
Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said
Mwambungu katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia iliyiadhimishwa kimkoa katika kijiji cha Lusonga Wilaya ya Songea.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAIDI MWAMBUNGU amekemea vikali
vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya wanawake katika mkoa wa Ruvuma.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha lusonga wilaya ya Songea hapo jana
MWAMBUNGU amesema ni marufuku wanaume kuuza mazao yao bila kushirikisha wake
zao. Na kwawale wanaotenda hivo watachukuliwa
hatua za kisheria kwa kuwa ni moja wapo ya ukatili dhidi ya wanawakePia amesema serikali inafanya juhudi ya kutokomeza
vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya wanawake.
Akisoma risala katika maadhimsho ya siku ya wanawake
iliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Lusonga wilaya ya Songea mkoani Ruvuma
afisa maendeleo ya jamii wa wilaya WENISARIA SWAI amesema kuwa katika mkoa wa
Ruvuma wananawake ndio wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula na biashara
lakini hawashirikishwi katika kutoa maamuzi.
Amesema wanawake wengi katika familia wananyimwahaki ya
kushirikikatika kutoa maamuziya mgawanyo wa mapato yanayopatikana ingawa wao
ndio wazalishaji na watendaji kazi wakubwa.Aidha shughuli nyingi zinazofanywa
na wanaake hazina ujira hali inayosababisha ndoa kukosa malezi mema hatimaye
watoto na vijana kuondoka nyumbani na kujiingiza katika makundi ya ombaomba
mitani.
Naye mwenyekiti wa kamati ya wafanyakazi wanawake wa chama
cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (talgwu) taifa dokta ANGELINA SANIKE ametoa
wito kwa jamii kuelimsha watoto kike ili kuondokana na mfumo dume .
Kwaundani zaidi bofya hapa http://demashonews.blogspot.com/2013/03/mkuu-wa-mkoa-wa-ruvuma-said-mwambungu.html