Saturday, February 23, 2013

TBC YATOA MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI SHULE YA UHURU MCHANGANYIKO

001Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (katikat) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana kuhusu maktaba hiyo wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam leo. Wengine ni Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mang’enya (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa tatu kushoto) na wafanyakazi wengine wa Vita Foam, TBC na walimu wa shule hiyo.
Shirika la Utangazaji nchini (TBC) pamoja na Kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited, leo wamekabidhi msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya shilingi Milioni 3 kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es Salaam. Msaada huo ni sehemu ya marejesho ya faida inayoipata kwa jamii (CSR).
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana amesema Jamii inayo wajibu wa kusaidia makundi ya watoto wenye ulemavu nchini ili kuwapa faraja na wajione nao ni sehemu ya jamii.
003Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto) moja ya nyenzo zinazotumiwa na
wanafunzi walemavu kuandikia wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam jana.
004Mkutubi msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto) moja ya kompyuta zinazotumiwa na wanafunzi walemavu kusomea wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya
sh milioni 3, Dar es Salaam jana. 
006
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi moja ya mashine inayotumiwa na watoto walemavu wa macho kuandikia kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mang’enya wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam jana.
007
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi sehemu ya magodoro 100 yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa Mratibu wa Elimu Kata ya Gerezani, Seraphina Mdamu kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi walemavu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited walipokwenda kutoa msaada huo shuleni hapo, Dar es Salaam jana. Wengine ni Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mang’enya na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa pili kulia).

Tuesday, February 19, 2013

KAMPUNI YA GAME FRONTIERS OF TANZANIA WAMEFANIKIWA KUKAMATA NYARA ZA SERIKALI ZENYE THAMANI YA MILION MIAMBILI - NAMTUMBO.


Hawa ni wafanyakazi wa Game frontiers of Tanzania wakiwa wamebeba pembe za ndovu
Pembe za ndovu, Risasi na Silaha zilizokamatwa

Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni ya Game Frontiers of Tanzania akifanya mahojiano na Bw. Gerson Msigwa ambaye ni mtangazaji wa TBC.


Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA kwa kushirikiana askari wanyamapori wa Selou na Askari wa vijiji vinavyozunguka pori la Akiba la Selou wamefanikiwa kukamata meno ya tembo 15 yenye thamani ya milion miambili, Risasi 9, Bunduki moja aina ya RIFFLE 458 na Gobole moja ambavyo hutumika kuulia wanyama .

Doria hiyo imechukua takribani siku tatu katika pori la Akiba la Selou ikiwa ni sehemu ya kuwatafuta majangili wanaofanya mauaji ya wanyamapori katika pori hilo,
Akizungumza na mwandishi wetu Bw. Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni hiyo ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA, Amesema kuwa hiyo ni kujituma kutokana na motisha ya fedha anayoitoa mwezeshaji wa kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA ndio chachu ya mafanikio ya kukamata meno,bunduki na risasi.

 Akiendelea kuzungumzia tukio hilo Bw. Mohamed Mpapa amesmea baada ya majangili kuwaona Game Frontiers Tanzania wakiwa katika doria ndani ya pori hilo huku wakiwa wamekamilika kimapigano majangili hao waliweza kukimbia na kuacha nyara hizo baada ya kuona nguvu yao ni ndogo katika kupambana na kundi la doria.

Ameongezea kwa kusema Kampuni yake imefurahishwa na mafanikio na ushirikiano uliopo kati yao, Serikali na wanavijiji kukabiliana na ujangili unaoendelea kuwamaliza tembo katika Pori la Akiba la Selou pia ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kuwafichua majangili.

Nae Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la Selou Bw. Bernald Lijaji amesema Pembe zilizokamatwa ni 15 pamoja na Bunduki aina ya RIFLE 458,Gobole moja na Risasi 9 aina ya 458 vimekamatwa katika Doria iliyofadhiriwa na Mwekezaji wa Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA

Friday, February 15, 2013

SIMBA NA AZAM POKEENI BARAKA ZA TFF KWENYE MICHEZO YENU YA LEO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazitakia kila la kheri timu za Azam, Jamhuri na Simba ambazo zinaiwakilisha Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.



Azam inacheza na Al Nasir Juba ya Sudan Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaofanyika Jumamosi (Februari 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.



Nayo Jamhuri ya Zanzibar kesho itacheza na St. Georges ya Ethiopia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaofanyika Uwanja wa Gombani

MWANDISHI WA HABARI WA TBC GERSON MSIGWA SIKU ALIPOKEA TUZO YA MWANDISHI BORA WA HABARI ZA POLISI KWA MKOA WA RUVUMA

  Mwandishi wa TBC Gerson Msigwa akipewacheti cha pongezi kutokana na juhudi za kutangaza kazi zinazofanywa na Jeshi la Polisi bila kuegemea upande wowote, Katikati ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedit Kazielege Nsimeki na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.


 Gerson Msigwa akiwa na Mke wake Catherine Nyoni wakiwa katika nyuso za furaha
 Gerson Msigwa akipunga mikono kuwasalimia wageni waalikwa

LEO HII SAA 5:00 AM KATIKA KIPINDI CHA MAISHA YANGU

Habari ya Asubuhinwapendwa? Naomba muungane nami itakapotimu saa 5:00 AM leo kupitia 98.7 TBC SONGEA nitakuwa katika kipindi cha maisha yangu na Kijana Hamidu ambaye kapitia magumu ya kuskitisha na kwawale waliokosa sehemu ya kwanza nawapa pole sana na leo hii tutakuwa sehemu ya Pili . karibuni sana nikupitia hapa hapa Tbc Songea...............