Sunday, January 20, 2013

MKUU WA WILAYA ASEMA "SACCOS NI SURUISHO LA AJIRA"

mkuu wa wilaya ya songea JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI akihutubia walimu wanachama wa SACCOS ya walimu manispaa ya songea
Jamii imetakiwa kutambua kuwa vyama vya kuweka na kukopa yaani SACCOS ni moja ya vyombo ambavyo vinaweza kupanua wigo wa ajira nchini kwa kuajiri vijana wanaotoka vyuoni katika kada mbalimbali na kuondo ukubwa wa tatizo la ukosefu wa ajira.

hayo yamaemwa na mkuu wa wilaya ya songea JOSEPH JOSEPH MKIRIKITI wakati wa mkutano mkuu wa SACCOS ya walimu wa manispaa ya songea


Aidha mkirikiti amewataka viongozi wanao shughulikia mikopo wawatumikia wananchi na sio watumikiwe na wanao hitaji mikopo kwa kufanya hivyo wataweza kuimarisha uhai wa chama na kukifanya kisonge mbele.

akisoma risala kwa mgeni rasmi makamo mwenyekiti wa saccos ya walimu manispaa ya songea JULIE LUOGA amesema chama kinakabiliwa na changamoto ya wanachama kutorudisha mikopo kwa wakati pamoja na wanachama wanao daiwa kutorudisha pesa mkononi pindi wanapochelewa kukatwa madeni yao na hazina.

Pia katika mkutano ho pia umefanyika uchaguzi wa kuchagua wajumbe saba wa bodi pamoja na mwenyekiti huku mwl.B.NCHIMBI akiibuka kidedea kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa jumla ya kura 221 huku JULIE LUOGA akichaguliwa tena kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho.