Friday, November 30, 2012

MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA MKOA WA RUVUMA AHAIDI KUTOA MADAWATI NA KUSAIDIA UPATIKANAJIWA ENEO LA UJENZI WA SHULE

 
  Mwenyekiti wa umoja wa vijana chama cha mapinduzi CCM Khalfan Kigwenembe ametoa ahadi hiyo ya kuchangia madawati baada ya risala ilyosomwa shuleni hapo na Mwalimu mkuu wa shule Bi Otilia Mbano kuonesha shule inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa madawati na kusababisha wanafunzi hao kukaa chini wakati wa masomo
Akipokea risala kutoka kwa mwl/mkuu
Aidha aliwataka wazazi wa watoto hao kuhakikisha watoto wao wanajiunga na Darasa la kwanza mapema ifikapo  mwaka 2013 ilikuendeleza masomo yao nakufika mbali kielimu huku akitoa mchango wa madaftari kwa wahitimu wote ili kuwapunguzia wazazi mzigo wa kununua vifaa vya kujifunzia pindi watakapo jiunga na darasa la kwanza,hata hivyo bwn:Kigwenembe amehaidi kuwa tafutia eneo la ujenzi wa shule hiyo kwani kwasasa shule hiyo inatumia majengo ya kupanga. 
 
 Akikabidhi vyeti kwa wahitimu
katika mahafari ya tisa ya shule ya mtakatifu teresia iliyopo bombambili mjini Songea wanafunzi 48 wamehitimu elimu ya awali na kutunukiwa vyeti.
 Nibaadhi ya wazazi wakiangalia kwaya kutoka kwa wahitimu ambao ni watoto wao.

Sunday, November 4, 2012

ALIYEKUWA BALOZI WA MSUMBIJI NCHINI TANZANIA AKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYENYE THAMANI YA TSHS MILIONI 1.2 WILAYANI TUNDURU - RUVUMA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj_SoB4QDRm6_WYHUBlluDCwWyKb7Yvsbryqi9GwIQkTgjUl0Eer8WeNrWUXdXqj88qlMB_pRkphz23ckv54miM3BjemfTCKqWY2wXZY64sWVsjSn9GUCQ7b6Cz5cxOL54361Do5teCljdZ/s1600/balozi.jpg 
Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Amour Zacarias Kupela (kulia) Picha maktaba
Na, Steven Augustino, Tunduru 
Aliyekuwa Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Bw.Amour Zacarias Kupela amekabidhi msaada wa vifaa vya Kusomea vyenye thamani ya Shilingi Milioni 1.2 kwa wanafunzi 500 wa Shule ya sekondari masonya zikiwa ni juhudi za nchi yake kudumisha urafiki na Tanzania.

Msaada huo uliotolewa na kiongozi huyo  ni madaftari makubwa (Counter Book 500), Peni 500 na Pensel 500 na Mipira 5 umetolewa kutokana na mapenzi ya Balozi huyo ambaye pamoja na mambo mengine ameahidi kuenzi kumbu kumbu za wapigania uhuru wa nchi ya Msumbiji na eneo ambapo ilianzishwa Jumuiya ya Umoja wa wanawake wa Msumbiji (OMM) march 16/1973. 

Akikabidhi Msaada huo kwa niaba ya Balozi Kupela  katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania Bw.Daniel Rui Simao Ntada alisema kuwa msaada huo ni mwendelezo wa ahadi ya Balozi huyo aliyo itoa wakati alipofanya ziara ya kuaga viongozi wa Wilaya ya Tunduru ambapo aliahidi kuisaidia Shule hiyo iliyopo katika eneo la kambi ya wapigania uhuru wa Chama Cha Frelimo Nchini Msumbiji .

Akifafanua taarifa hiyo Bw. Rui alisema kuwa Balozi Kupela alitoa ahadi hiyo wakati alipotembelea katika eneo hilo muhimu kwa historyia ya wapigania uhuru wa Nchi yao ambapo palikuwa ni miongoni mwa kambi kubwa za wapigania uhuru wa nchi yao wakiwemo Kamarada Samora Machel, Marcelino Dos Santos, Rais wa sasa Armando Guebuza, Dkt. Edward Mondlane na wengine wengi.

Katika taarifa hiyo pia Bw. Rui kwa niaba ya Balozi Kupela alisema Msaada huo ni juhudi za Balozi huyo kuendeleza kudumisha urafiki wa nchi hizo pamoja na kutunza, kuyahifadhi maeneo yote ya kumbu kumbu na kuenzi historia ya Tanzania na Msumbiji.

Bw. Rui alibainisha kuwa Kwavile Chama cha Frelimo Kilianzishwa Tanzania kwa kutoa baadhi ya maeneo ya ardhi yake kwa Chama hicho Cha Frelimo ambapo wapigania Uhuru hao walijenga Kambi za Kijeshi katika maeneo ya Nachingwea,Kongwa,Bagamoyo,Masonya na katika Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara ili wapigania uhuru  waendelee kutibiwa .

Mwl. Ngaunje katika hotuba yake pia alipokea mwaliko wa kupeleka Wanafunzi wa Shule yake katika Ziara ya kubadilishana taaluma katika Shule ya Sekondari Mekula iliyopo  Mkoa wa Niasa Nchini Msumbiji

Wasemaji wengine katika hafla hiyo walikuwa ni Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilaya ya Tunduru Mwl. Ally Mtamila mwakilishi wa Afisa elimu Shule za Msingi Wilayani humo Mwl. Kerlen Kitosi ambao pamoja na kumpongeza Balozi Kupela kwa msaada huo pia walipongeza juhudi zake za kuendeleza elimu ya Tanzania.

BW. OSMUND NA PAMELA WAMELEMETA -SONGEA

Bw.Osmund na Bi.Pamela wakiwa kanisani
Bibi harusi Pamela akiwa na Msimamiza wake Mh. Jenista Mhagama -Mbunge wa Jimbo la Peramiho 
Bi Pamela akiwa Kanisani
Bw.Osmund na Bi.Pamela wakiwa kanisani pamoja na wasimamizi wao


Bw.Osmund akijiandaa kumvisha pete Bi.Pamela 
Bw.Osmund akimvisha pete Bi.Pamela 
Bi.Pamela wakiwa kanisani akimvisha pete mumewe



Mh. Jenista Mhagama -Mbunge wa Jimbo la Peramiho akisaini