Friday, September 14, 2012

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA NA WAANDISHI WA HABARI MKOANI RUVUMA..














SIKU YA MAADHIMISHO YA YEBO SALAMA SONGEA




Ni baadhi ya madereva   yebo mjini Songea wakiwa kwenye maandamano yaliyofanyika siku ya tar..8..9..2012 katika viwanja vya majimaji majira ya saa.8 mchana chini ya uzamini wa ROTARY CLABU YA SONGEA na mgeni Rasmi alikuwa na mkuu wa wilaya ya Songea Mh: JOSEPH JOSEPH MKILIKITI



 Baadhi ya madereva yebo yebo (boda boda) wakiwa katika pozi ndani ya uwanja wa majimaji mjini Songea

Mgeni rasmi akiwasili katika viwanja  vya majimaji Mh: JOSEPH JOSEPH MKILIKITI siku ya ufunguzi wa yebo salama mjini Songea


Rais wa klabu ya Rotary ya Songea Dr. VENANCE MUSHI akisoma risala ya Rotary klabu ya Songea kwa mgeni rasmi Mh: JOSEPH JOSEPH MKILIKITI Mkuu wa wilaya katika ufunguzi wa mradi wa yebo salama-manispaa ya  songea

Mh; mkuu wa wilaya JOSEPH JOSEPH MKILIKITI akiwa katika pozi siku ya ufunguzi wa mradi wa yebo salama -manispaa ya Songea

Akijibu risala ya wana Rotary klabu ya songea



Akiwa kwenye maojiono na waandishi wa habari songea siku ya ufunguzi wa Rotary klabu ya Songea .

Monday, September 3, 2012

AJALI YA MOTO ILIYOTEKETEZA WATOTO WANNE - TUNDURU


Na Steven Augustino, Tunduru
WATOTO wanne wa familia moja wamefariki dunia baada ya miili yao kuteketea kwa kuunguzwa kwa moto uliozuka katika chumba wanancho lala.
Kufuatia hali hiyo Mama yao Mzazi Bi.Asha hamadi aliyedaiwa acha Mshumaa ukiwaka na kuwafungia watoto hao amelazwa katika Hospitali ya serikali ya Wilaya akiwa hakitambui kutokana na kuugua ugonjwa wa moyo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa kuwa chanzo cha moto huo ni mshumaa ambao uliachwa ukiwa unawake hukuwazazi wao wakiwa wamewafungia kwa nje na kulala chumbani kwao.
Watoto hao Marehemu kutoka katika familia Kipemba walitambuliwa  kwa majina ya Harid Nasoro (7),Hamid Nasoro  (5)Ally Nasoro(4) na  Alkam Nasoro(3).
Akizungumzia tukio hilo Baba wa Marehemu hao Bw. Nasoro Hamadi alidai kuwa  Watoto wake walipatwa na mkasa huo baada ya kufungiwa kwa nje na mama yao mzazi Bi.Asha hamadi kutokana na kilichodaiwa kuwa walifanya hivyo ili kuwadhibiti wasitoke nje kutokana na utundu walio kuwa nao.
Alisema chanzo cha kuamua kulala na mshumaa huo kilitokana na watoto hao kuzowea kulala na mwanga huku siku hiyo Umeme ulizima baada ya Luku yake kwisha huku kukiwa na zuio la wateja wa huduma hiyo kutoluhusiwa kununua Umene kupitia huduma za Simu, M-pesa, Nmb Mobil kama ilivyo kuwa imezoeleka.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. deusdedit Nsimeki mbali na amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo
Kwa mujibu wa taarifa ya Mganga aliyeifanyia uchunguzi miili ya marehemu hao Dkt. Moses Nwahasunga amesema kuwa chanzo cha vifo hivyo kilitokana na miili yao kukosa hewa safi na kuungua vibaya baada y amoto huo kulipuka ndani ya chumba.
 Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Chande Nalicho ametuma salamu za lambilambi na kuitaka familia hiyo kuwa subira wakati huu wa majonzi makubwa yaliyowakuta.
Msiba huo ambao uliwasisimua watu wengi na kuzusha simanzi na vilio kila kona ya mji wa tunduru Miili ya watoto hao imezikwa katika makabuli yalipo katika mtaa wa mabatini mjini hapa mungu azilaze mahala pema roho za marehemu amina.

Saturday, September 1, 2012

SONGEA TBC 98.7 FM

KARIBU KATIKA KIPINDI CHA MCHANA TULIVU ITAKAPOTIMII SAA 12:00 PM . UNAPATA NAFASI YA KUTUMA SALAM KWA NJIA YA SIMU 0769126506 PIA UNAWEZA KUINGIA KATIKA PAGE YETU YA TBC SONGEA UKA LIKE NA VILE VILE UKATUPIA HAPA SALAM ZAKO NASI TUTAZISOMA BILA HIYANA, UTAKUWA NAMI Hamza Mashole aka De Masho Sambamba na Cathy

SONGEA TBC 98.7 FM

TBC SONGEA 98.7 FM tupo hewani kipindi kilichpo hewani ni Kipindi cha Mipasho kinaendeshwa nae Cathy akisaidiana na Rauph Mohamedi na Leo tunawapambanisha Mzee Yusuph na Babu Ayubu, waweza piga simu namba 0769126506 na kupiga kura yako pia unaweza piga kura yako hapa