Friday, August 31, 2012

MPENZI MSIKILIZAJI WA TBC SONGEA KIPINDI KILICHOPO HEWANI NIKIPINDI CHA MCHANA TULIVU WAWEZA PIGA SIMU NAMBA 0769126506 AU UKATUMA MSG KATIKA UKURASA WETU BASI NASI TUTAZILUSHA HEWANI MOJA KWA MOJA .98.7 FM

MPENZI MSIKILIZAJI WA TBC SONGEA KIPINDI KILICHOPO HEWANI NIKIPINDI CHA MCHANA TULIVU WAWEZA PIGA SIMU NAMBA 0769126506 AU UKATUMA MSG KATIKA UKURASA WETU BASI NASI TUTAZILUSHA HEWANI MOJA KWA MOJA .98.7 FM, SONGEA MJENGONI NI CATHY NA HAMZA AKA De Masho

Thursday, August 30, 2012

MGAO WA MAJI MANISPAA YA SONGEA WAANZA


Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka katika Manispaa ya SONGEA Mkoani RUVUMA imelazimika kuanza kutoa maji kwa mgao wa asilimia 30, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu hali kama hiyo iikumbe manispaa ya SONGEA katika miaka mitano iliyopita.
 
Mwandishi wa Habari wa TBC GERSON MSIGWA aliyetembelea vyanzo vya maji vya Mto LUHILA na Tank la wazi la MATOGORO ameshuhudia kupungua maji kwa kasi, kulikosababisha Mamlaka hiyo kukusanya Meta za Ujazo 7000 ikilinganishwa na meta za ujazo zaidi ya 11,000 ambazo hukusanywa kipindi kama hiki
 
Hata utiririka wa maji yanayoingia katika tanki la Maji la wazi la SOUWASA lilipo Matogoro hapa SONGEA ni wa kujikongoja mno, hali inayowatisha hata maafisa wa SOUWASA wenyewe. Engineer FRANCIS KAPONGO Mkurugenzi Mtendaji wa SOUWASA anasema hii haijapata kutokea tangu mwaka 2007.

                          Habari na Gerson Msingwa