Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Amour Zacarias Kupela (kulia) Picha maktaba
Na, Steven Augustino, Tunduru
Aliyekuwa Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Bw.Amour Zacarias Kupela
amekabidhi msaada wa vifaa vya Kusomea vyenye thamani ya Shilingi Milioni 1.2
kwa wanafunzi 500 wa Shule ya sekondari masonya zikiwa ni juhudi za nchi yake
kudumisha urafiki na Tanzania.
Msaada huo uliotolewa na kiongozi huyo ni madaftari makubwa (Counter
Book 500), Peni 500 na Pensel 500 na Mipira 5 umetolewa kutokana na mapenzi ya
Balozi huyo ambaye pamoja na mambo mengine ameahidi kuenzi kumbu kumbu za
wapigania uhuru wa nchi ya Msumbiji na eneo ambapo ilianzishwa Jumuiya ya Umoja
wa wanawake wa Msumbiji (OMM) march 16/1973.
Akikabidhi Msaada huo kwa niaba ya Balozi Kupela katibu Mtendaji wa
Jumuiya ya Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania Bw.Daniel Rui Simao Ntada
alisema kuwa msaada huo ni mwendelezo wa ahadi ya Balozi huyo aliyo itoa wakati
alipofanya ziara ya kuaga viongozi wa Wilaya ya Tunduru ambapo aliahidi
kuisaidia Shule hiyo iliyopo katika eneo la kambi ya wapigania uhuru wa Chama
Cha Frelimo Nchini Msumbiji .
Akifafanua taarifa hiyo Bw. Rui alisema kuwa Balozi Kupela alitoa ahadi
hiyo wakati alipotembelea katika eneo hilo muhimu kwa historyia ya wapigania
uhuru wa Nchi yao ambapo palikuwa ni miongoni mwa kambi kubwa za wapigania
uhuru wa nchi yao wakiwemo Kamarada Samora Machel, Marcelino Dos Santos, Rais
wa sasa Armando Guebuza, Dkt. Edward Mondlane na wengine wengi.
Katika taarifa hiyo pia Bw. Rui kwa niaba ya Balozi Kupela alisema Msaada
huo ni juhudi za Balozi huyo kuendeleza kudumisha urafiki wa nchi hizo pamoja
na kutunza, kuyahifadhi maeneo yote ya kumbu kumbu na kuenzi historia ya
Tanzania na Msumbiji.
Bw. Rui alibainisha kuwa Kwavile Chama cha Frelimo Kilianzishwa Tanzania kwa
kutoa baadhi ya maeneo ya ardhi yake kwa Chama hicho Cha Frelimo ambapo
wapigania Uhuru hao walijenga Kambi za Kijeshi katika maeneo ya
Nachingwea,Kongwa,Bagamoyo,Masonya na katika Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara
ili wapigania uhuru waendelee kutibiwa .
Mwl. Ngaunje katika hotuba yake pia alipokea mwaliko wa kupeleka Wanafunzi
wa Shule yake katika Ziara ya kubadilishana taaluma katika Shule ya Sekondari
Mekula iliyopo Mkoa wa Niasa Nchini
Msumbiji
Wasemaji wengine katika hafla hiyo walikuwa ni Afisa Elimu wa Shule za
Sekondari Wilaya ya Tunduru Mwl. Ally Mtamila mwakilishi wa Afisa elimu Shule
za Msingi Wilayani humo Mwl. Kerlen Kitosi ambao pamoja na kumpongeza Balozi Kupela
kwa msaada huo pia walipongeza juhudi zake za kuendeleza elimu ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment