Thursday, August 30, 2012

MGAO WA MAJI MANISPAA YA SONGEA WAANZA


Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka katika Manispaa ya SONGEA Mkoani RUVUMA imelazimika kuanza kutoa maji kwa mgao wa asilimia 30, ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu hali kama hiyo iikumbe manispaa ya SONGEA katika miaka mitano iliyopita.
 
Mwandishi wa Habari wa TBC GERSON MSIGWA aliyetembelea vyanzo vya maji vya Mto LUHILA na Tank la wazi la MATOGORO ameshuhudia kupungua maji kwa kasi, kulikosababisha Mamlaka hiyo kukusanya Meta za Ujazo 7000 ikilinganishwa na meta za ujazo zaidi ya 11,000 ambazo hukusanywa kipindi kama hiki
 
Hata utiririka wa maji yanayoingia katika tanki la Maji la wazi la SOUWASA lilipo Matogoro hapa SONGEA ni wa kujikongoja mno, hali inayowatisha hata maafisa wa SOUWASA wenyewe. Engineer FRANCIS KAPONGO Mkurugenzi Mtendaji wa SOUWASA anasema hii haijapata kutokea tangu mwaka 2007.

                          Habari na Gerson Msingwa

No comments:

Post a Comment