Mkutubi
msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi
Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (katikat) akimwelezea Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana kuhusu
maktaba hiyo wakati shirika hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro
ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye
thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam leo. Wengine ni Mkuu wa Shule
hiyo, Anna Mang’enya (wa pili kushoto), Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa
Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa tatu kushoto) na wafanyakazi wengine
wa Vita Foam, TBC na walimu wa shule hiyo.
Shirika
la Utangazaji nchini (TBC) pamoja na Kampuni ya magodoro ya Vita Foam
(T) Limited, leo wamekabidhi msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya
shilingi Milioni 3 kwa Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko, Dar es
Salaam. Msaada huo ni sehemu ya marejesho ya faida inayoipata kwa jamii
(CSR).
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC), Clement Mshana amesema Jamii inayo wajibu wa
kusaidia makundi ya watoto wenye ulemavu nchini ili kuwapa faraja na
wajione nao ni sehemu ya jamii.
Mkutubi
msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi
Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto) moja ya
nyenzo zinazotumiwa na
wanafunzi walemavu kuandikia wakati TBC kwa kushirikiana na kampuni ya
magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100
yenye thamani ya sh milioni 3, Dar es Salaam jana.
Mkutubi
msaidizi wa Maktaba ya Watoto wenye ulemavu katika shule ya Msingi
Uhuru Mchanganyiko, Joyce Nyamuhokwa (kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana (kushoto) moja ya
kompyuta zinazotumiwa na wanafunzi walemavu kusomea wakati TBC kwa
kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd walipokwenda
kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya
sh milioni 3, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi
moja ya mashine inayotumiwa na watoto walemavu wa macho kuandikia kwa
Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mang’enya wakati TBC
kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) ltd
walipokwenda kutoa msaada wa magodoro 100 yenye thamani ya sh milioni 3,
Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini (TBC), Clement Mshana akikabidhi
sehemu ya magodoro 100 yenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa Mratibu
wa Elimu Kata ya Gerezani, Seraphina Mdamu kwa ajili ya matumizi ya
wanafunzi walemavu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko wakati shirika
hilo kwa kushirikiana na kampuni ya magodoro ya Vita Foam (T) Limited
walipokwenda kutoa msaada huo shuleni hapo, Dar es Salaam jana. Wengine
ni Mkuu wa Shule hiyo, Anna Mang’enya na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu
wa Vitafoam, Justine Mwakalinga (wa pili kulia).