Na Steven Chindiye - Tunduru
Mkazi wa Kijiji cha Mbes Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma aliyetambulika
kwa jina la Seifu Jafari (Adumba)(18) ameuawa na wananchi wenye hasila
baada ya kumtuhumu kuiba simu.
Pamoja na mauaji hayo ya kinyama kufuatia kipigo alicho kipata pia
wananchi hao walimchoma moto.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa kabla ya kifo hicho marehemu
akiwa na wenzake waliiba simu 6 ambazo zilikuwa zikichajiwa katika
nyumba ya Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Chikomo aliyefahamika kwa
jina moja la Mwl. Komba katika kata ya Mbesa Wilayani humo.
Walisema baada ya kufanikisha wizi huo marehemu na wenzake waliondoka
kurejea Mbesa.
Baada ya Kijana huyo kupata taarifa kuwa anatafutwa na kundi la watu alianza kuwakimbia baada ya kuwaona hali ambayo
iliwafanya wapige kelele za kuomba msaada kwa watu wengine.
Akiongea kwa njia ya Simu Baba Mzazi wa marehemu Adumba, Bw.Jafari
Alifa alisema kuwa adhabu na kifo hicho ni stahili kwa Mwanae na
kwamba hali hiyo imetokana na ukaidi wa kusikiliza maneno ya wakubwa.
Alisema katika kuhakikisha kuwa kijana wao huyo analelewa katika
mazingira mazuri familia yao ilijitahidi kumuonya mara kwa mara
abadilishe tabia hiyo ya udokozi bila mafanikio.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw.
Deusdedit Nsimeki mbali na kuidhibitisha kuwepo kwake alisema kuwa
polisi wanaendelea kuchumguza chanzo cha tukio hilo.
Aidha kamanda Nsimeki alikemea tabia za wananchi hao wanaotumia
mwamvuli wa hasila kutenda uhalifu kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za
bianadamu na kwamba watuhumiwa wote watakamatwa na kufikisha katika
vyombo vya sharia.